Site icon A24TV News

MONDULI MAMBO SAFI WANCHI WAPATA MAJI SAFI NA SALAMA PAMPUU MPYA KUTOKA UFARANSA YAFUNGWA MBUNGE ASHUKURU SERIKALI

Na Geofrey StephenMonduli  .Arusha

Mbunge wa jimbo la Monduli Fredick Lowasa amiwa na mkurugenzi wa mamlaka ya maji auwsa na mwenyemiti wa halmashauri ya Monduli wa kiteta jambo 

Akizungumza mara baada ya pampu hiyo kuwasili nchini na kufungwa  Mbunge wa jimbo la Monduli Fredick Lowasa amesema kuwa ameshukuru  serikali  ya awamu ya sita ya Mh Rais Samia Sulubu Assan Kwa kutatua tatizo hilo kwani lilikuwa  ni kero Kwa wananchi kufuatia wananchi kuhangaika kutafuta Maji  umbali mku wa ususani wanawake walilazimika kutafuta maji Kwa  punda  hata maeneo ya mjini jambo ambalo lilikuwa ni changamoto sana kwao 
Mbunge amesema  takribani kata 3 ikiwemo Monduli juu, meserani,Engutoto na Lashaine walikuwa wameathirika Kwa sehemu kubwa ukizingatia  ni kata za mjini ila  ameipongeza Mamlaka Kwa kipindi hicho ambacho walifanikiwa kusambaza maboza ya maji Kwa wananchi ili kuwasaidia kuondoa adha Kwa akina mama
AMesema kuwa Monduli Sasa maji yatapatikana kwa uraisi ikilinganishwa na hapo awali  kufuatia pampu kubwa kutoka ufaransa  yenye uwezo wa kusukuma maji kilometa 40  kufungwa katika kisima Cha Seedfam Ngaramtoni mkoani Arusha Ambapo mradi huo wa miaka 20 uliletwa na mzee Lowasa kupitia mkopo wa IDB.
Ameipongeza Mamlaka ya Maji Auwsa na uongozi wake Kwa kuonyesha jitiada za kubwa za upatikanaji wa pam. aliloliomba tokea wakati wake wa kwanza wa  kampeni enzi za marehemu Dr Magufuli  jambo ambalo  mchakato huo  ulikuwa haujaanza hata Kwa Rias wa Sasa haikuwa ahadi yake  kwani mchakato wa upatikanaji wa maji eneo hilo haukuwa kwenye mpango Bali na Hai na maeneo mengine lakini mheshimiwa  Rais baadaye alipokea jambo Hilo na kulifanyia kazi.
Mbunge Fred Lowada amesema  kuwa Monduli ni eneo ambalo wananchi hawakuwahi kuona maji tangu enzi za uhuru ila Sasa mradi huu unaenda vizuri kwani mradi mkubwa billion 16 unaotaraji kutokea utawanufaisha Wana Monduli hivi karibuni.

Mwenyekiti wa  Halmashauri ya Monduli Isack Joseph ametumia fursa hiyo kumshukuru waziri wa maji Juma Aweso Kwa kufanikisha jambo Hilo pamoja na mkuu wa wilaya ya Monduli Joshua Nasari Kwa kuwezesha kupatikana kwa pampuu hiyo  kupitia serikali ya awamu ya 6 kwani Kila wakati wamekuwa wakiangalia namna ya kutatua tatizo hilo la maji katika wilya ya Monduli .

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Justin Rujomba na mwenyekiti wa halmashauri monduli katka eneo la kupampu maji .
mkuu wa wilaya ya Monduli Joshua Nasari  ametoa pole Kwa wananchi kwani hakuna aliyependa tatizo Hilo kujitokeza  kwani halikupangwa ila Monduli sasa tayari tatizo hilo limefika mwisho kufuatia kujengwa  kisima chenye uwezo wa kubeba Lita milioni 10 ambacho kimeshakamilika ambapo vijiji 13 vitanufaika na mradi huo.
Mkuu wa wilaya Monduli Joshua Nassari akimsikiliza mkurugenzi wa mamlka ya maji Auwsa kwa makini.
Na Ijulikane kuwa wilaya ya  moduli hakuna mradi wowote wa maji umewahi kufanyika  hivyo kutokana na  mradi  mkubwa wa mkoa wa Arusha wa zaidi Bilioni 520 serikali iliona kilio cha wananchi wa Monduli ikaamua kufanya mradi mdogo ndani yake  wa  billion 16 ambapo tangu miaka 20  ipite haukuwahi kutokea hivyo mapinduzi makubwa yanakwenda kwenye  vijiji 13 mpaka nanja.
mradi huo wa maji unaenda kuongeza kiwango Cha maji eneo la Monduli Mjini kwani mkandarasi ameshapatikana ambaye ni Jandu kwani anaaminika na siyo kampuni ya ubabaihaji hivi karibuni mkataba huo utakwenda kusainiwa.
Mh Nasari alitoa angalizo Kwa Mamlaka na wananchi kutunza miundo mbinu ya maji ili iweze kudumu Kwani pampu hiyo imegharimu kiasi Kikubwa Cha fedha ambapo aliwataka kutunza hicho kidogo walichopata wakati wakisubiri mradi mkubwa ujazo ambapo amewakumbusha pia wananchi kujitahidi kutatua changamoto za wananchi na siyo kupiga Kelele  Bali kuonyesha njia.
Mkurugenzi  wa mkoa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (AUWSA) Enginia  Justin Rujomba amesema kuwa anaushukuru uongozi wa wilaya ya Monduli Kwa kumpa ushirikiano mkubwa Kwa kipindi Chote ambacho pampu ilivyokuwa imeuungua ambapo amesema  kuwa huo ni mfano wa kuigwa  na ya kuwa  kunapotokea jambo viongozi wanapaswa kutatua changamoto na siyo kulalamika.
Mkurugenzi Rujomba amesema kuwa  Mamlaka pamoja na  Ruwasa wamejipanga kutatua changamoto ya ukosefu wa maji mji wa  Monduli ambapo wamefunga pampu mpya ili maji yaweze kupatikana licha ya mradi mkubwa ujao wa bilio16 ambao umeidhinishwa na mheshimiwa Rais ,
Mwisho .