Site icon A24TV News

NABII MKUU DKT GEORDAVIE AKABIDHI KANISA LA KISASA KWA MCHUNGAJI SABORE

Na Geofrey  Stephen Arumeru.

Katika hali ya kuendeleza kazi ya Mungu Nabii Mkuu Dokta GeoDavie amezindua kanisa la kisasa pamoja na kumkabidhi rasmi Mchungaji Jackob Sabore kwa lengo la kueneza injili ya neno la Mungu.

Akiongea na Maelfu ya waumini waliojitokzeka katika shughuli hiyo Nabii Mkuu amesema kazi ya Mungu itaendelea kubarikiwa kwa kuwa watumishi wengi kwa sasa wanatangaza injili kwa kuwapa furaha waumini pamoja na kusaidia kutatuwa matatizo yao katika maisha yao.

Zoaezi la kukabidhi kanisa kwa Sabore liliendana na utukufu wa kuwashika wajasiria mali mikono kwa mitaji ambapo zaidi wa wajasiria mali wapatao kumi na tatu walipatiwa mitaji na kupatiwa baraka ili kufanya kazi na kuinuka katika maisha yao ya kila siku .

Hii sio mara ya kwanza kwa Nabii Mkuu GeoDavie kuwashika watumishi wa Mungu kwa kuwajengea Makanisa bali ni muendelezo katika kutimiza maandandiko na kuwanyanyuwa wale wasio na nguvu ambapo pia katika uzinduzi huo wa kanisa amewataka watumishi mbali mbali kuwa na tabia ya kusaidia jamii katika maisha kwani kile wanacho pata sio cha kwao pekee yao.

Mwisho.