Na Richard Mrusha Geita
SERIKALI kupitia Wakala wa Nishati vijijini (REA) imefanikiwa kufikisha nishati ya umeme vijijini katika vijiji 10,987 ambayo karibu asilimia 89 ya vijiji vyote 12318 vilivyopo hapa nchini vimeshafikiwa na umeme.
Amesema na mapaka baadhi ya wakandarasi wapo saiti wanaendelea na kazi.
Amesema matarajio mpaka mwakani vijiji vyote vitakuwa vimeshafikiwa na umeme lakini vijiji vingi vitapata umeme kabla ya desemba mwaka huu na vingine mwakani.
“Kwa hiyo tukimaliza zoezi la kupeleka umeme vijijini tunahamia kwenye vitongoji ingawa mradi ya kupeleka umeme kwenye vitongoji tulikuwa tumeshauanza .”amesema.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo ,Tanzania Bara ina vitongoji 64,760 ambapo karibu vitongoji 28586 vimeshafikiwa na umeme kwa hiyo utakuja kuona kuna vitoingoji 36,000 ndio bado havijafikiwa na umeme.
“Kama mnavyofahamu Tanzania tumebarikiwa nchi yetu ni kubwa ,Tanzania peke yake ukijumlisha Kenya, Uganda , Ruanda na Burundi yaani Afrika Mashariki ya mwanzo,bado Tanzania ni kubwa lakini serikali imeweza kufikisha umeme kwenye eneo lote la nchi
“Kwa hiyo suala la umeme kwa kiasi kikubwa tumefanikiwa na sasa hivi kama unavyoona pamoja na kushughulika na umeme tunaingia kwenye nishati safi ya kupikia
Mwishoni mwa mwaka juzi Rais alizindua kongamano la Nishati ya kupikia ambapo katika kikao hicho aliagiza kuanzishwa kwa dira ya Taifa na Mfuko wa Taifa wa Nishati ya kupikia lengo lilikuwa ni kwa ajili ya kuhama kutoka kwenye njia na nishati ya asili ya kupikia kuja kwenye nishati safi na bora ya kupikia.
Ameongeza kuwa Kufuatia uzinduzi huo REA tumekuwa tukielimisha wananchi nchi nzima kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ambavyo vimekuwa ni chanzo cha ukataji miti hovyo na hivyo kufanya uharibifu wa mazingira.
Amesema,wamekuwa wakielimisha wananchi kuhusu athari na faida za matumizi ya nishati safi ya kupikia huku akisema madhara ni kusababisha uharibifu wa mazingira na kuleta mabadiliko ya Tabianchi.
Vile vlie amesema zipo athari za kiafya ikiwa ni pamoja na macho kuwa mekundu,athari kwa akina mama wajawazito lakini pia vifo .
“Kwa hiyo maeneo mengi hapa nchini tunaweza kuhama kwenye matumizi ya kuni na mkaa na kuingia kwenye nishati safi ya kupikia ambayo pia inasadia kuokoa misitu yetu ambayo wataalam wanatuambia tunapoteza misitu ya heka laki nne kwa mwaka lakini pia kuna vifo vinavyoadiriwa kufikia wastani wa 33,000 kwa mwaka kutokana na matumizi ya nishati ya kuni.
“Lakini pia bado kuna madhara mengine ya kiafya,mtu anaweza asife lakini kuna kuathirika macho,akina mama wajawazito wanaathirika lakini tuseme ni jambo ambalo lina athari kubwa sana .”amesisitiza
Amesema wakati umefika sasa kwa wananchi kuachana kupikia kuni na mkaa na kuhamia kwenye nishati safi ya kupikia kama vile gesi,umeme kwani serikali imeshaweka miundombinu hiyo.
Mwisho .