Site icon A24TV News

SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAWEKEZAJI SEKTA YA MADINI

Na Richard Mrusha Geita

KAMPUNI ya FEMA MINING AND DRILLING LTD inayojihusisha uchimbaji,ucholongaji na ulipuaji wa madini nchini imeshukuru serikali ya awamu ya sita(6) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Hassan Suluhu kwa kuwapa fursa na nafasi kampuni za kizawa kufanya kazi katika migodi nchini.

Akizungumza hayo katika maonesho ya sita ya kitaifa ya teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili Halimashauri ya mji wa mkoani Geita

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea kwenye baada lao Muhandisi Jackline Mtei amesem anapenda kumshukuru Rais DKT. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi kwenye sekta ya madini haswa kwa wazawa tofauti na huko nyuma.

amesema hivi leo tunaona mabadiliko makubwa kwenye sekta ya madini haswa sisi wazawa kwampata tenda kwenye makampuni makubwa na ya kati yanayoifanya shughuli za uchimbaji hapa chini na kupitia sisi tumeweza kuzalisha ajira na kuchangia katika jamii inayotuzunguka”, anasema Mtei.

Amesema wameendelea kupata zabuni kwenye migodi midogo ya kati pamoja na mikubwa,kwa Kupitia kampuni yao ya FEMA wao ni kampuni zawa kampuni ya kitanzania kwa hiyo meona mama alivyotengeneza mazingira ambayo yamewezesha kapata zabuni katika migodi ya kati na mikubwa”

Aidha,Jackline Mtei ameeleza fursa ya ajira kwa wanawake katika sekta ya madini amesema “kupitia kampuni hiyo imeweza kuwasaidia wanawake kupata ajira zaidi ya wanawake kumi na tano wamepata ajira akiwemo yeye


Kwa upande wake Afisa manunuzi na usambazaji FEMA MINING AND DRILLING LTD Frank Joseph amesema “FEMA wameweza kushirikiana na makampuni tofauti katika kuwapa zabuni katika kampuni yao kama vile usambazaji wa vipuri,oils na virainisha kwa ajili ya mashine zao pia huduma zingine tofauti tofauti kama za usafi,chakula na huduma nyingine za kijamii,Hivyo wameweza kuzalisha ajira kwa kampuni zaidi ya tano

Ameongeza kuwa kampuni hiyo tangu kuanzishwa kwake imekuwa ikifanya kazi kubwa na kwa ueledi na ndio maana imeendelea kupata zabuni kwenye makampuni yanayojihusisha na shughuli za uchimbaji hapa chini.

 

Mwisho .