Site icon A24TV News

SHULE BINAFSI NA MCHANGO WA KUKUZA ELIMU NCHINI AFISA ELIMU APENDEKEZA ZIPATE RUZUKU

Na Tumaini Mafie, Arusha
Afisa Elimu taaluma Jiji la Arusha Henry Mwakamisa asifu Shule binafsi jijini hapo na kusema zinaleta tija katika Elimu Kwa kuongoza ufaulu Kwa asilimia kubwa jijini hapo.

Aliyasema hayo katika Sherehe ya mahafali iliyofanyika shule ya msingi Tuishime mkoani Arusha ambapo alisema Shule binafsi zinachangia Kwa kiasi kikubwa ufaulu na kuliweka Jiji la Arusha katika nafasi ya kwanza Kwa miaka mitano mfululizo kati ya halmashauri ya 180 zilizoko nchini Tanzania.

” Tuna zaidi ya Shule 170 Jiji la Arusha na kati ya hizi 140 ni shule binafsi na hizi tukizungumzia ufaulu wa Shule zinachangia kwa asilimia kubwa sana ni rai yangu kuwa mtaendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi Ili Jiji letu liendelee kubaki katika rekodi nzuri ” alisema Mwakamisa.

Aliwataka Wazazi na walezi kuhakikisha kuwa wanawasaidia watoto waweze kufikia ndoto zao Kwa kuwahimiza kusoma Kwa bidii pindi wawapo nyumbani huku akisema watoto wanapoanza kusoma muda mwingi wanakuwa Shuleni na Muda mchache ndio wanakaa na Wazazi wao, na jukumu la Mzazi ni kulipa ada ,mahitaji muhimu Kwa watoto jambo ambalo linachochea watoto kuishi ndoto zao.

Naye mgeni rasmi katika hafla hiyo Beatrice Amani ambaye ni meneja wa Benki ya CRDB tawi la Njiro aliwataka wahitimu hao kuanza kuwaza matokeo gani watakatoyaleta katika Jamii Ili kuleta mabadiliko chanya katika Jamii wanazotoka

” Mnatakiwa kuwaza ni matokeo gani mtakayoiletea Jamii siku za usoni mara baada ya kumaliza masomo yenu na mtafanikisha jambo hili pale tu mtakapo mtanguliza Mungu na kusoma kwa bidii” alisema Amani.

Naye mkuu wa Shule hiyo Venance Nyari alisema Kati ya wanafunzi 348 wa Shule hiyo waliohitimu darasa la Saba ni 42 ambapo alisema Shule hiyo hutoa Elimu ya nadharia na vitendo Kwa ajili ya kumuandaa kijana kuweza kukabiliana na maisha.

Alitaja baadhi ya matatizo yanayoikumba Shule hiyo kuwa ni pamoja na Upumgufu wa vyumba vya madarasa, ukosefu wa Bweni litakaloleta ufanisi kwa wanafunzi wanaotoka mbali Ili waweze kujisomea Kwa uhuru ikiwa ni pamoja na kutokuwepo Kwa jengo la utawala.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shule hiyo Naomi Masenge aliwaasa wanafunzi waliohitimu kukazana katika masomo Yao na wakaiendelee kufanya vizuri kama walivyokuwa wakifanya walipokuwa katika Shule hiyo.

Mwisho