Site icon A24TV News

TASAC YAWANOA WADAU WA MADINI MKOANI GEITA MAJUKUMU YA KIPEKEE “EXCLUSIVE MANDATE”

Na. Costantine James , Geita

Shirika la uwakala wa meli Tanzania (Tanzania shipping Agency Corporation TASAC) wamewakumbusha wadau wa sekta ya madini wajibu wa TASAC kifungu Cha namba 7(1) Cha Sheria ya uwakala wa Meli sura 415 inayowapa TASAC majukumu ya kipekee “Exclusive Mandate” ya utoaji wa huduma ya uwakala wa forodha ,inatekeleza majukumu ya ukomboaji wa shehena katika maeneo mbalimbali ya forodha kwa bidhaa silaha na vilipuzi ,makinikia na kemikali zinazotumika kwenye kampuni za uchimbaji madini.TASAC wameongea hayo Leo Ijumaa September 29,2023 katika Maonesho ya sita (6) ya teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya Bombambili EPAZ mkoani Geita.

TASAC ni shirika la umma liloanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya uwakala wa meli nchini sura namba 415 na kuanza kutekeleza majukumu yake kuanzia 23 February mwaka 2018 ambayo ipo chini ya Wizara ya Uchukizi,TASAC ilianzishwa ili kudhibiti na kusimamia sekta ya usafiri wa majini (Bahari,maziwa,mabwawa na mito) ambayo inasimamia utekelezaji wa mikataba ya kimataifa ya shirika la Bahari Duniani(International Maritime Organization IMO) iliyoridhiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.TASAC inatoa huduma ya uwakala wa forodha katika bidhaa zilizoainishwa kisheria (Exclusive).

Akizungumza na waandishi wa Habari Afisa uhusiano Mwandamizi Amina Miruko amesema “TASAC ina majukumu mengi ambayo naomba niyataje majukumu hayo ni pamoja na kuhakikisha kusimamia na kudhibiti usafiri wa majini kwa kuhakikisha usalama wa vyombo ..vyombo vyenyewe,abiria,mizigo yao pamoja na mazingira yote ya usafirishaji,Sisi TASAC tunafanya kaguzi mbalimbali katika vyombo hivyo kuhakikisha kwamba hao wanaoendesha hivyo vyombo wanakuwa na utaalamu wa kutosha lakini sio hilo tu tunapofanya kaguzi pia tunakuwa tunahakikisha kwamba kunakuwa na vyombo vya usalama ili linapotekea tatizo lolote au dharura yeyote wa abiria wanaweza kuokolewa na kutoka wakiwa salama”

“TASAC inafanya kazi ya biashara ya meli,Katika biashara ya meli TASAC imekuwa ikifanya kazi katika maeneo kumi na Saba… kufanya uondoshaji wa shehena bandarini katika bidhaa kumi na Saba lakini kutokana na mabadiliko ya Sheria ikapelekea ikapunguziwa na kufanya kazi katika maeneo matano ambayo tu ambapo maeneo hayo ambayo pia inatufanya tuwepo hapa Leo ni Makanikia,ni vipuri ama mashine mbalimbali ambazo zinatumika kufanya uchimbaji Madini na migodini lakini vile vile kemikali zote ambazo zinatumika kufanya uchimbaji katika maeneo ya migodi lakini sio hilo tu pia ni silaha na virupuzi”

Kwa upande wake Afisa udhibiti huduma za bandari kutoka TASAC Victoria Miyonga amesema “Moja ya jukumu kubwa la TASAC ambalo limepewa kisheria ni kuhakikisha kuwa Kuna udhibiti Bora katika huduma zinazotolewa katika bandari pamoja na usafirishaji kwa njia ya maji jukumu Hilo tunalifanya kwa mujibu wa kifungu Cha kumi na Mbili Cha Sheria ya uwakala wa meli sura ya 415 katika kutekeleza jukumu Hilo malengo makuu ya udhibiti kwanza kabisa ni kuchochea ushindani baina ya watoa huduma ili kuhakikisha kwamba wanatoa huduma ambazo zenye tija na Bora