Site icon A24TV News

WANAFUNZI WAIMIZWA MASOMO YA UBAHARIA NA UHANDISI KUONDOA CHANGAMOTO YA WATAALAM

Na Geofrey Stephe,Arusha

VIJANA wanaohitimu masomo yao mbalimbali kwenye vyuo wapewa mbinu za kuachana na utegemezi wa ajira za serikali, badala yake wajiunge na kozi ya ubaharia na  uhandisi zenye watalamu wachache duniani, ili kupata ujuzi utakaowasaidia kujiajiri na kuajiriwa kiurahisi.

Ushauri huo umetolewa Jijini Arusha na  mmoja wa Wataalamu wa masuala ya ufuatiliaji na tathimini kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Watu Wenye Ulamavu,James Mallya, wakati akizungumza na vyombo mbalimbali  vya habari, katika kongamano  la pili  la kitaifa, la wiki ya ufuatiliaji  na tathimini.⁷

Alisema  kwa Tanzania vijana hawana sababu ya kukosa mafunzo hayo, sababu tayari kuna Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) ambacho kinatoa kozi hizo na kusaidia vijana wengi wanaohitimu kuajiriwa kwenye vyombo vya majini ndani na nje ya nchi, sababu ya uchache wa wataalamu hao.

“Ifike mahali  vijana wetu waachane kuoma masomo ya kupangiwa na wazazi wao au ndugu, bali waangalie soko la ajira, hizi kozi wataalamu wachache wa ubaharia, ukisoma lazima utapata kibarua au utajiajiri mwenyewe kwenye bahari zetu na maziwa na kuondokana na kulalamikia serikali juu ya ajira,”alisema.

Alisema  kozi hiyo inafundisha kijana kupata ujuzi hata wa uokoaji majini, hivyo  akiwa na ujuzi huo hawezi kukosa kazi ya kufanya hata kwa kujiajiri, pamoja na kupata fursa ya kwenda nje ya nchi kupata uzoefu zaidi na kuachana na utegemezi wa serikali au wazazi.

Naye Makamu Mkuu wa  Chuo cha Bahari Dar es Salaam, kwenye Idara ya  Mipango, Fedha na Utawala, Dk.Lucas Mwisila alisema  chuo hicho kinazalisha wataalamu pia wenye uwezo wa kufanya ufuatiliaji,tathimini, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu ili kuleta matokeo chanya kazini.

“Lengo la kutoa kozi zenye wataalamu wa aina hii ili kuwezesha jamii kupata huduma zenye tija kwao na Taifa, sababu pale unapofanya kitu bila kufanya ufuatiliaji na tathimini huwezi jua kama kizuri au la  na unapofahamu kasoro zake zinarekebishwa mapema na kutoa huduma zinazokidhi vigezo vinavyohitajika katika jamii,”alisema

Pia alisema moja ya faida za  wataalamu kuzingatia ufuatiliaji na kufanya tathimini, husaidia  mazao yanayopatikana ndani ya bahari, kama mwani,mafuta, umeme  au samaki, yote yafike katika masoko kwa wakati.

Mwisho.