Site icon A24TV News

WAZIRI PROF ADOLF MKENDA AZINDUA MPANGO WA ELIMU KWA MAENDELEO ENDELEVU , PONGEZI KWA UNESCO na UNICEF

Na Geofrey Stephen A24Tv

Uhitimishaji wa namna ya kuwa na Muongozo wa Elimu kwa ajili ya maendeleo endelevu, jambo hili lipo katika Mpango wa nchi za SADC na Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kuwa na Muongozo huo kwa nchi hizo.

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda Ameyasema hayo septemba 22 2023 katika Uzinduzi wa Mpango wa Elimu kwa maendeleo endelevu uliofanyika Jijini Arusha ambapo ameyashukuru mashirika ya Umoja wa Mataifa UNESCO na UNICEF kwa kushirikiana na serikali kuandaa Mpango huo.

Alisema nchi za SADC kupitia mawaziri wa Elimu walikutana na kuipa Kazi UNESCO ya kuratibu miongozo hiyo kwa nchi zote za SADC,Aidha Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kumaliza uandaji wa Muongozo huo baada ya kukamilika ndio wamekutana kuupitia kwa ajili ya matumizi.

Alisema Kazi yake kuu ya Muongozo huo ni kuona Elimu inayotelewa inawaandaa vijana kuelewa changamoto za mazingira Mabadiliko ya tabianchi na maendeleo endelevu kwa ujumla wake.

kwa Mujibu wa Prof.Mkenda alisema bahati nzuri sana Muongozo huu inaakisi Yale ambayo yapo katika Rasimu ya sera ya Elimu na Mafunzo ya Amali 2014 Toleo la 2023 ambalo tunatarajia kutoka siku za karibuni kwa kweli hii ni kama mkakati wa serikali.

Alisema Muongozo huo ni kama mkakati wa serikali kwa maendeleo endelevu na ni muhimu sana kwa Dunia inavyoenda Sasa hivi changamoto tunazoziona Mabadiliko ya tabia nchi hasa Mabadiliko ya jinsi mvua zinavyonyesha wakati mwingine Joto likiwa Kubwa sana baridi Kali sana hivyo suala hilo ni muhimu likiwa ni sehemu ya Elimu tunayoitoa na Elimu ya vitendo mafunzo ya Amali.

Alisema katika Muongozo huo nchi za SADC zilikubaliana kwamba ni muhimu sana kuangalia masuala ya viwanda masuala ya kilimo na masuala ya uwekezaji nk. na hayo kwa kwetu sisi kwenye sera ya Elimu na Mafunzo ni masuala yaliozingatiwa.

Elimu yetu ambayo tunaitoa ya mafunzo ya Amali kwa Sasa hivi tutawaandaa vijana wetu katika mambo ya viwanda na katika masuala mbalimbali yanayoendana na ujasiriamali kwa hiyo tunafurahi hatimaye sisi tunao Muongozo na inawezekana ndio nchi ya kwanza kukamilisha Kazi hii ya Muongozo huu.

Awali Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bwana. Michel Toto
amesema UNESCO imeridhika kushirikishwa katika uandaaji wa Muongozo huo na inayofuraha kuwa sehemu ya kukamilisha zoezi hilo muhimu kwa maendeleo ya bara la Afrika hususani nchi za SADC.

Alisema Zoezi hilo wameshirikiana na pande zote za SMT na SMZ kupitia wizara za Elimu Maliasili na Mazingira hivyo Muongozo huo utasaidia kutoa Elimu sahihi kwa vijana waangali skuli Hadi kuwa na kizazi kinachokuwa na Elimu yenye tija katika maendeleo endelevu na utunzaji wa mazingira.

Kwa Upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali SMZ Salim Abdullah amesema kwamba kwa Upande wa Zanzibar Mpango huo utasaidia kukabiliana na Mabadiliko ya uelewa mdogo wa Jamii kwa kushirikisha wanafunzi wangali skuli kupitia mafunzo ya Amali.

Amesema athari za mazingira na Mabadiliko ya tabianchi yamepelekea kuongezeka na kupunguza uzalishaji kwa baadhi ya vyakula na maji kuongeza Joto pamoja na magonjwa ya wanadamu wanyama na mimea Hali hizo zinaathiri ukuaji wa mtoto hivyo kupelekea taifa kutokuwa na Afya.

Mwisho .