Site icon A24TV News

DKT.KIRUSWA AMEFUNGUA MKUTANO WA SITA WA MWAKA WA WAKANDARASI WALIOWEKEZA KATIKA MADINI YANAYOPATIKANA CHINI YA SAKAFU YA BAHARI KUU 2023.

Na Richard Mrusha

NAIBU Waziri wa madini Dkt.Steven Kiruswa amefungua mkutano wa siku tatu wa wakandarasi waliowekeza katika madini yanayopatikana chini ya sakafu ya bahari kuu 2023 na utajadili agenda mbalimbali kuhusu masuala ya utafiti ,uchimbaji ,na utunzaji wa Mazingira yaliyo chini ya sakafu ya bahari kuu.

Amesema mkutano huo ni kuendelea na utekelezaji wa Article 145 kwenye UNCLOS 1982 na makubaliano ya mwaka 1994 kuhusu shughuli za uchimbaji wa madini kwenye sakafu ya bahari.

DKT Kiruswa ameyasema haya leo octoba 22, 2023 jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano huo ambapo Amesema pamoja na kuwa nchi wanachama wa umoja wa mataifa zinaendelea kutoa kuandaa kanuni zitakazosimamia uvunaji wa rasilimali hizo japo nchi nyingi Dunia zinawasiwasi kuhusu madhara ya kimazingira yanayoweza kusababishwa na shughuli za uchimbaji wa madini hayo.

“Nimuhimu Sasa nchi yetu ya Tanzania ikiwa ni Moja kati ya nchi 169 wanachama kuendelea kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu rasilimali madini chini ya sakafu ya bahari ili kunufaika na rasilimali hiyo ambayo ni Moja ya maeneo muhimu ya uchumi wa buluu.”Amesema Kiruswa

Nakuongeza kuwa ” Niukweli usiopingika kuwa sekta ya madini ni nguzo muhimu na ni Chachu ya maendeleo Duniani kote,hivyo ili madini yetu yaweze Kubadilisha uchumi wa nchi na maendeleo ya wananchi Wizara inaendelea kusimamia shughuli za sekta ya madini ili kuhakikisha kuwa zinafungamanishwa na sekta nyingine za kiuchumi .”Amesema.

“Mimi na viongozi wenzangu wa Wizara tumejiwekekea maono yenye kauli mbiu ya isamayo ” Vision 2030 madini ni Maisha na Utafiti ” kupitia kauli mbiu hii Wizara umelenga kufanya utafiti Kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya High Resolution Geophysical Survey angalau kufikia asilimia 50 ya eneo la nchi nzima ifikapo mwaka 2030″amesisitiza

Ameongeza kuwa gharama za utafiti huo ni kubwa na Kwa Sasa Wizara inatafuta fedha kutoka Kwa wadau wa maendeleo na Serikali ili kuiwezesha Taasisi ya jiolojia na Utafiti wa madini Tanzania GST kutekeleza jukumu hilo.

“Ni Imani yetu kwamba baada ya kufanyika Kwa utafiti huo tutafahamu tabia na aina mbalimbali za miamba nchini yenye viashiria vya uwepo wa madini mbalimbali kutokana na uwepo wa taarifa hizo za kijiolojia uwekezaji katika sekta ya madini utaongezeka kwani itakuwa rahisi taarifa hizo kutumika kufanya utafiti wa kina katika maeneo mbalimbali ya nchi na hivyo kuongeza fursa kuanzishwa Kwa uchimbaji madini hapa nchini .”Amesema Dkt Kiruswa

Nakuongeza kuwa “mpango huu utawezesha pia Serikali kuendesha programu za uchorongaji na Utafiti wa kina katika maeneo yenye viashiria vya madini Kwa ajili ya wachimbaji wadogo ili kujua Kwa uhakika mashapo ya madini yaliyopo katika maeneo yao

Amesema Kwa miaka wachimbaji wamekuwa wakitengwa na kuchimba madini katika maeneo ambayo taarifa za kijiolojia hazijulikani na hivyo kuendesha shughuli zao Kwa kubahatisha uchimbaji wa aina hiyo umekuwa hauna tija kwao .

“Kwakuwekeza na kufahamu taarifa za kijiolojia katika maeneo ya kutafanya wachimbaji wadogo waendeshe shughuli zao Kwa uhakika nakuongeza mchango wao katika uchumi wa taifa mambo yote haya niliyoyaeleza ndio yanayobeba na kutafsiri kauli mbiu “Vision 2030 Madini ni Maisha na Utafiti

Mwisho.