Site icon A24TV News

Emirates imezindua vifaa vipya vya huduma kwa abiria vyenye kuonyesha spishi za wanyama pori zilizo hatarini kutoweka.

Na Mwandishi waA24Rv

Dubai, Oktoba 2023

Shirika la Ndege la Emirates linachukua hatua kubwa katika ahadi yake ya uhifadhi wa mazingira na uhifadhi wa wanyama pori kwa kuwasilisha vifaa vya huduma vipya na bure kwa abiria wake wa madaraja ya Premium Economy na Economy katika safari ndefu ulimwenguni. vifaa hivi vya huduma vitakavyopatikana kwenye ndege ni matokeo ya ushirikiano wa pekee na umoja wa wanyamapori, ilioundwa kutoa ufahamu juu ya baadhi ya spishi za wanyama zilizo hatari kupotea zaidi duniani.

Uhifadhi wa wanyama pori na mazingira ya asilia umekuwa moyoni mwa Mfumo wa Uhifadhi wa Mazingira wa Emirates kwa muda mrefu. Uzinduzi na mkusanyiko huu mpya wa vifaa vya huduma unathibitisha ushirikiano wa muda mrefu wa Emirates na umoja wa wanyama pori na dhamira yake ya kuongeza ufahamu juu ya spishi zilizo hatarini na kudhibiti biashara haramu ya wanyama pori na bidhaa za wanyama.

Pochi na vifungo vya vitabu katika vifaa vya huduma zitaonyesha michoro ya baadhi ya viumbe wanaotiliwa mashaka kupotea na waliovushwa katika biashara haramu ya manyama pori duniani, ikiwa ni pamoja na kasa wa bahari wa kijani, tembo wa Afrika, Gorilla, Papa kichwa-nyundo, Simba, Pangolin, na kifaru mweusi.

Umoja wa wanyama pori ulitoa takwimu za kushtua, ikisisitiza uzito wa suala hili. kwa ulimwengu mzima, ambapo ilidai Tembo 100 wanauawa kila siku, huku kiwango cha sasa cha uwindaji haramu kinaweza kupelekea kutoweka kwao porini ifikapo 2025. Hadi sasa kuna vifaru 30,000 pekee waliosalia porini, kutoka katika idadi ya vifaru 500,000 waliokuwepo mwanzoni mwa karne ya 20, huku Pangolin wakiwa wanyama wanaosafirishwa zaidi ulimwenguni.

David Fein, Mwenyekiti wa Umoja wa wanyama pori, alitoa maoni yake akisema, “Biashara haramu ya wanyama pori ni uhalifu ulioandaliwa kimataifa unaosukuma spishi maarufu kote ulimwenguni kuelekea kutoweka kwa kasi ya kutisha. Shirika la ndege Emirates wanatoa huduma ya usafirishaji wana jukumu kubwa katika kuvuruga minyororo ya usambazaji na usafirishaji haramu wa wanyamapori. Emirates wamekuwa wakionyesha uongozi na dhamira katika kukabiliana na tishio hili la ulimwengu. Tunafurahi kuona vifaa vya huduma vipya vya Emirates vilivonakishiwa kwa picha za wanyamapori sasa zinapatikana kwenye ndege na tunatumai kwamba abiria watapata habari na msukumo katika vifaa vya huduma.”

Emirates imekuwa ikihusika kikamilifu katika vita dhidi ya biashara haramu ya wanyama pori na unyonyaji pia ni mwanachama wa Umoja wa Kikosi Kazi cha Usafiri wa Wanyamapori. Shirika la ndege Emirates lina sera ya kutovumilia kabisa biashara haramu ya wanyama pori na bidhaa za wanyama. Idara yake ya mizigo, Emirates SkyCargo, imetekeleza marufuku kamili kwa usafirishaji wa nyara za uwindaji kwa Tembo, Kifaru, Simba, na Tigri. Mnamo Juni 2023, Emirates ilithibitisha dhamira yake ya uhifadhi wa mazingira kwa kupata vyeti vya Tathmini ya Mazingira ya IATA (IEnvA) Hatua ya Kwanza katika moduli ya Biashara Haramu ya Wanyama ya IEnvA.

Pochi za wanyama za Emirates zinaweza kutumika tena na zimeundwa kutokana na karatasi inayoweza kuoshwa, ambayo inaonyesha sanaa ya wanyama hao walioko kwenye hatari ya kutoweka duniani zilizochapishwa kwa wino usiokuwa na sumu. Yaliyomo yanajumuisha seti ya vitu vya kusafiri vyenye thamani vilivyotengenezwa kutokana na vifaa vinavyopunguza matumizi ya plastiki mpya kwa kutumia plastiki iliosindikwa tena baada ya kutimika. Sufuria ya meno imeundwa kutoka kwa mchanganyiko wa kisamvu cha ngano na plastiki.

soksi na kipande cha kuvalia macho vimeundwa kutoka kwa plastiki iliyosindikwa tena baada ya kutumika.

Emirates pia itarejesha vipuli vya masikio kwenye amenity kits mwishoni mwa mwaka – kufuatia maombi ya wateja.

Mwisho