Site icon A24TV News

LATRA ARUSHA .YAWATAKA MADEREVA KUFUATA KANUNI NA TARATIBU ZA USALAMA BARABARANI

Na Geofrey Stephen Arusha.

Wamiliki wa vyombo vya usafiri mkoani Arusha wamekutana kwa  pamoja na Latra Tira na Jeshi la polisi na kufanya mazungumzo zaidi ya  juu ya sheria za usafirishaji.

Pichani ni afisa Latra mkiwa Arusha Bwana Joseph Michael

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kikao hicho afisa wa latra mkoa wa Arusha Joseph Michael amesema kuwa lengo la mazungumzo hayo ni kupeana elimu na  ufafanuzi wa sheria kanuni na taratibu za usalama barabarani.
 
Amesema kuwa mara baada ya elimu hiyo mkoa wa Arusha unategemewa kuwepo Kwa ufanisa mkubwa na  mabadiliko makubwa katika sekta ya usafirishaji.
 
Afisa Latra huyo amesema kuwa kuanzia tarehe 1/10 Hadi tarehe 14/10 madereva wote  Kwa mujibu wa sheria no 5 kifungu Cha kwanza E madereva  wanapaswa  kusajiliwa na kuthibitishwa na Latra Kwa madereva wenye Madaraja ya leseni  C C1,C2 C3 na E 
 
Wamiliki wote wamekumbushwa kutuma maombi mapema kabla ya leseni zao kuisha kwenye mfumo wa Rim ili waweze kupata leseni ambapo mtu binafsi anapaswa kuwa vielelezo vifuatavyo ikiwemo namba ya Nida,kopi ya kadi ya gari,kopi ya hati ya bima,na ukaguzi wa polisi.
 
Madereva ili waweze kusajiliwa  wanapaswa kuwa na Nida, cheti Cha mafunzo na leseni ambapo ametoa wito  Kwa wamiliki wote kuhakikisha wamefuata utaratibu huo.
 
Mrakibu mwandamizi wa jeshi la polisi Bi Sauda Mohamed  mkoani arusha amewashukuru wadau waliotoa elimu pamoja na wamiliki waliohududhiria katika mafunzo hayo ambapo amewataka madereva kutoa ushirikiano pindi wanapokutana na changamoto mbalimbali kwani amesema kuwa 
ofisi yake ipo wazi na wasaidizi wapo ili kutatua changamoto wanazokabiliana nazo pindi wapo barabarani.

Pichani ni Mrakibu mwandamizi wa jeshi la polisi Bi Sauda Mohamed  mkoani arusha

Mwenyekiti wa kamati iliyoundwa na wamiliki wa daladala  Gerald Muniss amesema kuwa lengo la kuundwa kamati hiyo ni kushirikiana na  taasis za serikali lengo likiwa ni  kuangalia kuona namna gani kufanya usafiri huo kuwa wa kisasa zaidi 

Pichani ni mwenyekiti wa kamati ya Daladala Bwana Gerald Muniss

Hata hivyo wamiliki wengi walionekana kukosa uelewa kuhusu mambo ya usafirishaji  kutoka latra,bima pamoja na Tra ndio maana semina hiyo imeandaliwa ambapo semina hiyo imeonekana kuwafungua.
 
 Afisa Bima  Caroline Modest  kutoka Mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania  TIRA Kanda ya kaskazini Amesema kuwa changamoto kubwa inayowakabili kukata Bima Kwa ada pungufu ambapo wakati mwingine hukuta kupitia chombo binafsi ili hali bima Ile inaenda kutumia kwenye gari la abiria.
Pichani ni Afisa Bima Kanda ya kaskazin  Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tira Bi Caroline Modest ku