Site icon A24TV News

MKUTANO WA ASASI WANGURUMA JIJINI ARUSHA JAMII YATAKIWA KUKUBALI MABADILIKO YA KIDIGITAL

Na Mwandishi wa A24Tv Arusha

Kishindo cha wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaanza kunguruma Jijini Arusha mapema leo  ikiwa na wadau wa kutosha  na  kuanza kuamasisha jamii kupokea mabadiliko ya  teknolojia na kutumia katika kunufaisha jamii .

Mkurugenzi  wa Foundation for Civil Society Francis Kiwanga akiongea katika mkutano huo amesema kuna kila namna kukubali teknolojia katika kutambua changa moto zake na faida zake ambazo zimekua chachu ya maendeleo kwa watanzania na jamii kubwa Duniani

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Francis Kiwanga akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa simba Aicc 

Mada nyingine ni ujumuishwaji na uwezashaji kidigitali, matumizi ya takwimu katika kuleta manufaa katika jamii, teknolojia na utetezi katika jamii, elimu na mafunzo ya kidigitali nchini Tanzania, teknolojia kwa maendeleo endelevu pamoja na kuimarisha usalama mtandaoni.


Mwakilishi wa shirika la Apple Inc kutoka nchini  Marekani ambaye ni Mtanzania, Aboubakar Ally amesema mabadiliko ya kiteknolojia ya kidigital  duniani kwa sasa imekua kwa kasi  kubwa sana na matokeo mazuri hivyo jamii  iwe tayari katika mabadiliko ya kidigital  na kupenda kutumia

Mwisho .