Site icon A24TV News

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI ARIDHISHWA NA MABORESHO YA KIWANDA CHA NDEGE KISONGO ARUSHA

Na Geofrey Stepehen Arusha

Naibu Waziri wa Uchukuzi David kihenzile aridhishwa na maendeleo, usimamizi na maboresho yanayoendelea kwenye uwanja wa ndege wa Arusha ikiwemo jengo jipya la abiria na sehemu ya kuruka na kutua ndege.

Akizungumza Jijini Arusha wakati wa muendelezo wa ziara zake za kuongea na Uongozi na Kukagua Miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania(TAA) amesema Tanzania ni ya pili Kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii duniani ambapo asilimia 80 ya watalii hupita kaskazini huku Arusha ikitumika kama lango hivyo ukilishwaji wa Run way yenye mita 1880 Toka 1680 za awali na sehemu ya kugeuzia ndege na jengo jipya la abiria vitachochea ongezeko la wageni na watalii.

“Sambamba na maboresho yanayoendelea Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya mambo mawili makubwa kuongeza eneo la kurukia ndege Kwa Mita 200 ambapo awali lilikuwa na Miata 1680 na Sasa 1880, ujenzi wa jengo jipya la abiria lililofikia asilimia 92, maegesho ya ndege yameboreshwa, mindombinu ya kuingia uwanjani na sehemu ya kugeuzia ndege ambapo sasa ndege kubwa zitafika” amesisitiza Kihenzile.

 

Kihenzile amesema uwanja wa ndege wa Arusha unahudumia watu 296,000 Kwa takwimu zilizopo na miruko yake inafika 39,000 Kwa mwaka hivyo ni kiwanja muhimu Kwa uchumi wa taiga letu kwani watalii wengi wanakuja hapa Kwa ndege zao binafsi hata za abiria wanakwenda kwenye vivutio vyetu vya utalii hasa hapa kaskazini ambapo ndiyo lango kuu la utalii.

 

“Unapozungumza kiwanja hiki Cha Arusha ndiyo kitovu Cha watalii Kwa ndege za saizi ya kati ukiacha ndege kubwa za kimataifa hivyo ukamilifu wa hili eneo la kurukia ndege ambalo Lina sehemu za kugeuzia ndege na Jengo la abiria lenye uwezo wa kuhudumia abiria 1,000 Kwa mara Moja vitainua sana uchumi wa Arusha Kwa kuongeza watalii zaidi na kuongeza Pato la taifa” amesisitiza kihenzile.

Pamoja na hayo amesema Kwa upande wa maboresho ya eneo la maegesho ya magari ambalo limekamilika kinachofanyika ni kuongeza uwezo wa jengo la abiria lenye sehemu ya kukaa abiria na VIP za kutosha, sehemu ya kuingia na kutoka abiria , ni jengo zuri na la kisiasa maana kulikuwa na jengo dogo ila maono ni makubwa ya kuhudumia abiria laki Sita Kwa mwaka.

Vilevile kihenzile ameielekeza mamalaka ya Viwanja vya ndege kuhakikisha miradi iliyobaki inakamilika mara moja ili iende ikahudimie watanzania na kuwataka changamoto zote ambazo ni za kiwizara na kiserikali ziletwe Wizarani haraka.

Naye Kaimu Meneja wa Kiwanja Cha Ndege Cha Arusha Zaria Waziri amesema jengo jipya la abiria linategemewa kukamilikwa mwezi wa 12 mwaka huu na limefikia asilimia 92 mpaka Sasa, mradi wa ujenzi wa Barbara ya kuingia kiwanja, maegesho ya magari na ndege, na mfumo wa kupaki magari vimeshakamilika hivyo wanategemea kupata watalii wengi zaidi ambapo jengo likikamilika litahudumia abiria 1,000 Kwa siku na laki Sita Kwa mwaka na wanategemea kuweka taa ili uwanja utumike masaa 24.

Mwisho.