Site icon A24TV News

RAIS WA AZAKI SERIKALI ITUSAIDIE KATIKA KUTAMBUA MCHANGO WA TAASISI ZETU KUPATA UFADHILI

Na  Geofrey Stephen .

Asasi za kiraia(Azaki)zimeomba Serikali kuweza kuwatofautisha na asasi binafsi Kwa kuwa Mpaka sasa bado kuna mwingiliano mkubwa hasa kwenye masuala ya wafadhili..

Hayo yameelezwa na Rais wa taasisi ya foundation for civil society Dkt Stigmata Tenga wakati akifunga mkutano wa Azaki uliokuwa unafanyika jijini Aruha.

Amesema kuwa lengo la asasi zisizo Za Kiserakali pamoja na Azaki zote zipo Tanzania lakini malengo ni tofauti

Alifafanua kuwa Kwa kushindwa kutofautisha asasi hizo imepelekea baadhi ya wafadhili kupeleka fedha Kwa asasi hizo Huku Azaki kushindwa Kupata Haki zao

“tunaomba tusaidiwe Kwa kuwa kuna agenda nyingi Ambazo tumeshindwa kuzikamata, na sauti yetu ni Moja tu”aliongeza

Katika hatua nyingine alisema kuwa Azaki imejipanga katika kuhakikisha kuwa wanaendelea kuboresha mambo yao ikiwa ni pamoja na kuwa na matamasha kila Mwaka Ili waweze kujifunza.

“mwakani tutaasogeza matamasha ambapo mabadiliko yote yanalenga kuwafanya washiriki waweze kufuraia Lakini,pia kujifunza na kuongeza ufanisi zaidi”

Mwisho