Site icon A24TV News

RM KYANDO YALETA KICHEKO KWA WACHIMBAJI WADOGO

Na Richard Mrusha Geita.

Mkuu wa Idara ya Mosoko kutoka Kampuni ya R.M.Kyando Edger Chifupa amesema Kampuni imedhamiria kuwainua wachimbaji wadogo kiuchumi kwa kuwauzia mitambo ( Mashine ) ya kisasa ya uchimbaji wa Madini Kwa Bei nafuu ili waweze kutimiza ndoto zao kiuchumi.

Hayo ameyasema jana wakati wa mahojioano Maalum na vyombo mbalimbali vya habari waliotembelea banda lao kwenye Maonesho ya sita ya Kimataifa na Teknolojia ya Madini yaliyofanyika katika Viwanja vya EPZA Bombambili Halmashauri ya Mji wa Geita 2023.

Chifupa amesema Kampuni ya R.M. Kyando inajishughulisha na uuzaji wa Vifaa mbalimbali vya Uchimbaji wa Madini ambapo ipo katika Mikoa minne kwa hapa nchini.

Aidha Chifupa amesema iwapo wadau mbalimbali walaoielewa kauli Mbiu ya Mwaka huu 2023 ” Matumizi ya Teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi wa Mazingira. Geita ” wasingewaletea mitambo ama Mashine za mabilioni ya pesa huku walijua wazi kuwa wachimbaji wadogo hawana hizo fedha za kununulia vifaa vya gharama kubwa kiasi hiko.

“Tunaamini hadi tunaondoka hapa uwanjani Wachimbaji wadogo na wale ambao wanatamani kuwa wachimbaji ambao walikua wanaogopa kuingia katika shughuli za uchimbaji, wakijua kwamba kupata vifaa vyake ni gharama kubwa sana, Kampuni ya R.M.Kyando tumewaletea Teknolojia rahisi sana na ya kisasa, ambayo sasa naamini baada ya Maonesho haya watu watamiminika katika Ofisi zetu katika matawi yote nchi nzima ili waweze kujipatia bidhaa zetu nawaende wakachimbe kisasa ili wainue uchumi na hatimaye waweze kuendana na kauli Mbiu isemayo Matumizi ya Teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi Mazingira” amesema Chifupa.

Kufuatia hilo amesema utoaji wa teknolojia Kwa wachimbaji wadogo utaongeza tija katika shughuli zao na hatimaye kuweza kubadilisha maisha yao, zitabadilisha maisha ya jamii Tanzania kwa ujumla.

“Ukichagua kufanya kazi na sisi utakua umechagua na tuseme One stop Center Mining, maana ikifanya kazi na sisi kwanza utajiopatia Teknolojia ya vifaa , pili sisi ni wauzaji wakubwa wa kemikali za uchechuaji pia utazipata kwetu, tatu kwetu sisi ukiija unapima sampuli maana tunayo Maabara ya kisasa kabisa ya upimiaji sampuli, na pia vifaa ukininua kwetu na tunatoa na warantii , sio hizi Kampuni za mfukoni hapana ” amesema Chifupa.

Aidha amefafanua kuwa wao wana maeneo Maalum, na hivyo sio kwamba wakikuuzia Leo, ndio maana wanaingia sokoni ” With Confidence” kwamba wanauza kitu ambacho wanakiamini, na hivyo ndio maana wanatoa warantii ya kati ya mwezi 1- 3.

” Kampuni yetu ina miaka 7 sokoni toka tulipoianzisha 2016-2023 hukunikiwa na Wafanyakazi zaidi ya 30 katika Mikoa 4 nchini hadi sasa tuna matawi 5, na matawi 2 katika Mkoa wa Mbeya ( Chunya na Mji Mdogo wa Makongolosi ) tunayo matawi Mkoa wa Songwe, tunayo matawi Shinyanga ( Kahama) na Kwa Mkoa wa Geita ( Katoro ) amesema Chifupa.

Akizungumzia kuhusiana na uwepo wao katika Maonesho hayo na namna walivyoyaona kwa upande wao amesema wao ni mara yao ya kwanza kushiriki, ambapo wameyafurahia sana, ni Maonesho makubwa ukiachia Maonesho ya sabasaba Kwa nchi hii Maonesho makubwa zaidi yanayofuatia ni haya ya Madini ya siku 10 ( September 20-30, 2023).

Hata hivyo ameongeza kuwa kuwepo kwao katika Maonesho hayo wamepata muda wa kuonyesha bidhaa zao Kwa kipindi chote Cha siku 10, wametembelewa na wageni wengi mbalimbali, wamepata muda wa kutoa elimu ya bidhaa wanazouza Kwa wachimbaji na jamii kwa ujumla.

 

Mwisho