Site icon A24TV News

TAASISI ZA KIRAIA ZAJIKITA ARUSHA KUJADILI CHANGAMOTO ZA MIFUMO YA KIDIGITAL ,HUSUSANI KWA WANAWAKE

Na Geofrey Steohen Arusha.

Taasisi mbalimbali za kiraia zinatarajia kukutana jijini Arusha kwa kujadili na kutatua changamoto mbalimbali zinazoathiri mifumo ya techenolojia kwa lengo la kuimarisha na kuboresha SEKTA hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa kituo cha sheria na Haki za binadamu Dkt Anna Henga amesema changamoto inayowaathiri wananchi ni pamoja na kukosekana  kwa mtandao hasa vijini na kukatika kwa umeme mara kwa mara.
Na hiyo upelekea jamii kubwa kukosa mawasiliano jambo ambalo linarusha nyuma maendeleo hususani katika kuwasikiana na kuwasilisha changamoto zinazo wakabili kwa kukosa mawasiliano muhimu ya kidigital
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya wiki Azaki Nesia Mahenge ameeleza mambo yatakayojadiliwa Katika mkutano huo ambapo ni pamoja kauli mbiu ya mwaka huu ni Teknolojia na Jamii, ambapo wataangalia katika masuala ya teknolojia wapi walipotoka na wanapokwenda.

Amefafanua kua  malengo ya mkutano huo ni kuimarisha uhusiano kati ya serikali na sekta binafsi, ikiwemo kuweka mikakati ya Azaki katika kutekeleza miradi kupitia teknolojia.

Naye Mchambuzi wa kijinsia kutoka mtandao wa jinsia Deogratius temba amesema watahakikisha wanawake wanawezeshwa kutumia technojia bila kubagiliwa.
Mwisho.