Site icon A24TV News

TEITI YAWATAKA WADAU, WANANCHI KUJA KUJIFUNZA

Na Richard Mrusha

WADAU wa sekta ya madini na wananchi kwa ujumla wameshauriwa kuitumia Taasisi ya TEITI iliyopo chini ya Wizara ya Madini kutambua fursa mbalimbali zinazopatikana.

Hayo yamesemwa na Ofisa wa TEITI, Erick Katagory wakati akizungumza na mwandishi wa habari katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo kunafanyika Jukwaa la Kimataifa la Uwekezaji wa Madini Tanzani.

Katagory amesema TEITI inashiriki jukwaa hilo muhimu kwa sekta ya madini, hivyo wanawaomba wananchi na wadau kujitokeza kwa lengo la kupata taarifa za sekta hiyo.

Amesema makampuni yote ambayo yameshiriki kwenye mkutano huo ni wadau wa TEITI hivyo wanakazi kubwa kuweza kupata taarifa zao mbalimbali ili wananchi waweze kuzifahamu.

Amesema jukwaa hilo ni fursa kubwa Kwa TEITI kuweza kutoa taarifa kwa wananchi lakini pia wananchi wenyewe waweze kutumia nafasi hiyo kujifunza hasa kuhusu madini.

Amesema wananchi wanapaswa kujua taarifa zipi za msingi ambazo mtu anaweza kuzitumia na lengo kubwa ni kuweza kuona ambavyo Serikali yao inafanya kuiboresha sekta hiyo.

“Hadi kufikia leo tumetoa ripoti 13 na ripoti ya mwisho imetoka mwezi June mwaka huu ambapo ripoti hiyo imelinganisha makampuni 45 kwa maana makampuni yote ambayo yanajihusisha na mafuta , gesi asilia na mengine”amesema.

Ameongeza kuwa ripoti hizo zipo wazi hivyo ni jukumu la msingi wananchi wakatembelea kwenye banda lao ili kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Taasisi ya TEITI .

“Taasisi ya TEITI ni Taasisi ambayo ipo chini ya Wizara ya Madini na ilioazishwa mwaka 2009 baada ya nchi ya Tanzanaia kujiunga na umoja wa kimataifa ya uwazi na uwajibikaji,”amesema .

Amesema wananchi wanahaki ya msingi wa kuelewa taasisi yao inafanya kazi gani na hilo ndio jukumu lake kubwa na kuleta uwazi na uwajibikaji hivyo Taasisi hiyo ilitoa ripoti hizo ambazo zinakuwa na mambo mbalimbali na kubwa zaidi ni sera ya madini,gesi asilia mbalimbali.

Ameongeza kuwa wadau wanaendelea kupata uelewa kuhusu Taasisi hiyo na kimsingi taarifa zinawafikia kuhusu majukumu ya Taasisi hiyo.

Mwisho