Site icon A24TV News

USIKU WA MADINI WAUPAMBA MKUTANO WA KIMATAIFA

Na mwandishi wetu

Waziri wa Madini nchini Malawi Mhe. Monica Chang’anamuno amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi na mikakati mbalimbali anayofanya katika kuendeleza Sekta ya Madini nchini.

Mhe. Chang’anamuno alitoa pongezi hizo Oktoba 25, 2023 katika hafla ya Usiku wa Madini uliyoambatana na utoaji Tuzo kwa wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini waliofanya vizuri ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini mchango wako kwenye maendeleo na ukuaji wa sekta.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe.Chang’anamuno alisema kuwa mazingira halisi yanaonesha kuwa Rais Dkt. Samia anaendelea kufanya juhudi nyingi sana katika kuendeleza Sekta ya Madini kwa kushirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Serikali.

Akielezea kuhusu Mpango wa Wajibu wa Migodi kwa Jamii inayozunguka Mgodi (CSR) , Mhe. Chang’amuno aliipongeza kwa kuwepo Mpango mzuri unaounganishwa na Sera ya Madini katika kutoa fursa za kiuchumi kwa watanzania kushiriki katika uchumi wa madini.

Mhe.Chang’anamuno aliongeza kuwa amejifunza mengi kuhusu shughuli za uongezaji na kueleza kuwa ataishauri Serikali ya Malawi kuhusu kuwepo wa Kituo cha mfano katika utoaji mafunzo ya uongezaji uhamani nchini Malawi kama ilivyo kwa Kituo cha Uongezaji Thamani Madini Tanzania cha TGC.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Anglo Ashanti kampuni iliyokuwa mdhamini Mkuu wa hafla ya Usiku wa Madini Terry Strong, akitoa hotuba fupi alisema kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa maendeleo ya sekta ya madini.

Katika usiku huo zilipata tuzo kupitia vipengele mbalimbali ikiwemo Utunzaji wa Mazingira Migodi, Tuzo ya Ukataji na Uongezaji Thamani Madini, Ulipaji wa Mapato ya Serikali, Uwezeshaji wa Ushiriki wa Wananchi katika Sekta ya Madini, Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii zinazozunguka Migodi, Mwanamke bora katika uchimbaji wa madini , Mshindi Bora katika Kujenga na tiuzo maalum kwa mtaalam aliyetoa mchangomkubwa katika sekta ya madini ambapo Kamishna wa Tume ya Madini Prof. AbdulKarim Mruma alipata tuzo kama Mtaalam wa Geoscience katika ukuzaji wa sekta ya madini na maendeleo ya nchi.

Kampuni zilizoshinda katika usiku huo kupitia ushindi mbalimbali ni pamoja na Twiga Minerals Corporation, Shanta Gold, Ako Group, GGML,Appex resources, Ruvuma Coal Limited, Jitegemee Holding, The Tanzanite Experience na Leminatha Colonel Kabigumila.

Wakati huo, huo, Miss Tanzania Mwaka 2023 Halima Kopwe alikuwa kivutio katika hafla ya Usiku wa Madini wakati wa Onesho la Vito na bidhaa za mapambo ambapo pamoja na warembo wengine walipata fursa ya kupita jukwaani kuonesha bidhaa za madini ya vito na usonara kutokana na madini mbalimbali yanayozalishwa na bidhaa mbalimbali za vito na usonara zinazotengenezwa na kampuni za ndani.

Kampuni zilizoonesha madini yake ni pamoja na Gem Point, Gem Tanzanite,Ruvu Gemstone, Tanzania Gemological Centre (TGC) na Facet Gems

Mwisho