Site icon A24TV News

WANANCHI TUMIENI BODI YA NAFAKA KUPATA CHAKULA BORA

Na Richard Mrusha Geita

AFISA mauzo na usambazaji kutoka Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko Kanda ya ziwa Francisco Amos Amesema kuwa walikuwa ni moja ya Taasisi ya Serikali ambayo walishiriki maonesho ya madini mkoani Geita nakwamba kwao yamekuwa yamafanikio makubwa.

Amesema kuwa wananchi wengi walipata fursa ya kufika kwenye Banda lao na Kwa ujumla walipenda huduma na bidhaa ambazo walikuja nazo kwenye maonesho hayo.

Amos ameyasema hayo septemba 30 mwaka huu katika hitimisho la maonesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya madini ambayo yanafanyika Kila mwaka mkoani humo .

Amos Amesema licha ya kwamba ni mara yao ya kwanza kushiriki kwenye maonesho hayo lakini yamewapa picha nzuri kwamba wakati mwingine waje vizuri zaidi nakwamba wananchi wamependa bidhaa na huduma na wameonyesha uhitaji mkubwa zaidi.

“Kwakifupi naweza kusema maonesho yamekuwa tofauti na tulivyotarajia kwani tulikuja kama kuona kama bidhaa watazipenda lakini kimsingi majibu yamekuwa mazuri na wametembelea wengi na bidhaa zimechukuliwa za kutosha na tumepata mawakala wa kutosha na wasambazaji wengine wakutosha.”Amesema Amos.

Ameongeza kuwa meseji kubwa ambayo inapelekwa Kwa wanageita na Kanda ya ziwa ni kwamba hasa wakulima na wadau wote ambao wanahusika katika sekta ya nafaka na kilimo Kwa ujumla ni Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko imetengenezwa maalumu au kuundwa maalumu Kwaajili ya kuja kuwa Jukwaa litakalokuja kuwanufaisha wakulima .

Ameongeza kuwa anatoa wito Kwa wakulima waendelee kulima mazao ya kisasa waendelee kuboresha mashamba yao na vitu mbalimbali vinavyotumika kwenye kilimo ili waendelee kupata mazao ya kutosha kwani Soko la bidhaa zao lipo na Bodi ya nafaka ni Jukwaa muhimu sana na lina maana sana ambapo wao wanaweza kuuza mazao yao hivyo wanageita na watanzania waendelee kulima na baada ya hapo bidhaa zao zipo kwenye supermarket na maduka mengine zitapatikana na Kwa Bei nafuu kabisa .

“Uhakika wa bidhaa upo na wakati mwingine tutakuja vizuri zaidi na bidhaa nyingi ambazo wananchi wameziulizia na kuhusu changamoto wananchi wengi wanakosa elimu ya kutosha hasa inapofika suala la ubora wa chakula na wanamitazamo furani kuhusu ubora wa chakula hivyo wakati mwingine tutakuja vizuri zaidi na kuwaeleza wananchi kuhusu ubora wa chakula lakini pia kuwajengea uwezo wa uelewa zaidi .

Mwisho