Geofrey Stephen ARUSHA
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa umma,George Simba chawene,ametoa siku 14 Kwa Maafisa raslimali watu kwenye halmashauri na Idara zingine za umma kuhakikisha watumishi wote wenye madai mbalimbali walipwe kwa kuwa Serikali ilishapekela fedha Vinginevyo watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Agizo hilo amelitoa wakati alipokuwa akifungua kikao kazi cha siku tatu cha Wakuu wa Idara za Utawala na rasilimali watu,Taasisi za Umma Sekretarieti za Mikoa na mamlaka za serikali za Mitaa kwenye Ukumbi wa mikutano wà kimataifa AICC,Jijini Arusha,na kueleza kuwa kikao hicho kitumike kubadilisha uzoefu ,kukumbushana ,kubadilishama uzoefu na mbinu kwa ajili ya kuimarisha Utumishi wa umma na usimamizi wake.
Aidha Simbachawene alisisitiza kuwa watumishi wa umma wanao wajibu wa kutekeleza majukumu yao kwa misingi ya sera ,Sheria,kanuni na taratibu na miongozo mbalimbali na kuhakikisha watumishi wa umma wanapata haki zao za kiutumishi kwa a wakati.
Alisema,Serikali imeshatoa fedha za madai mbalimbali ya watumishi wa umma,lakini kuna baadhi ya Maafisa raslimali watu wamekuwa wakianzisha michakato mingine na hivyo kusababisha watumishi wenye madai kutolipwa hivyo akamtaka Katibu mkuu wa Wizara hiyo kufuatilia na kuchukua hatua sitahiki dhidi ya afisa raslimali watu anaekwamisha malipo hayo.
Simbachawene,amewatahadharisha Maafisa raslimali watu kuwa hatasita kuwachukulia hatua wale wote ambao itabainika kwenye maeneo yao kuna mapungufu hivyo watekeleze majukumu yao ipasavyo Ili kuepuka kuleta madhara Katika Utumishi wa umma.
Niendelee kusisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili kwa kuwa tumeendelea kupokea malalamiko kuhusu vitendo vya uvunjifu wa maadili ikiwemo Rushwa, lugha zisizofaa, kufanya udanganyifu wa nyaraka ikiwemo kughushi barua za masuala mbalimbali ya kiutumishi kama uhamisho wa kwenda sehemu zenye maslahi mazuri.
“Hivyo, nitoe wito kwa wote wanao jihusisha na tabia hiyo kuacha mara moja na hatua kali zitaendelea kuchukuliwa kwa wahusika. Vilevile, katika eneo hili la uhamisho ipo tabia ya baadhi ya Waajiri kukataa kuwapokea watumishi wanaohamishiwa kwenye Taasisi hizo na baadhi kutoruhusu watumishi kuhama hata pale inapoelekezwa na Mamlaka.
“Suala hili ni kinyume na Sheria, Kanuni na Taratibu kwa kuwa kitendo hicho ni kukosa utii kwa Serikali pamoja na Mamlaka zilizo juu yao. Nawaelekeza waajiri wa aina hii waache tabia hizo”
Alisema kuwa jumla ya watumishi wote wa Serikali na umma wapatao 600,000, wamelipwa nyongeza ya mishahara,watumishi 120,210. walipandishwa madaraja na kuwabadisha kada watumishi 8080 na madeni mbalimbali yamelipwa lakini madeni yamebakia kwenye Serikaliza mitaa kutokana na Maafisa raslimali watu kuanzisha michakato mipya ambayo haipo.
Alisema utafiti uliofanywa mwaka 2022 umebaini kuwepo matumizi mabaya ya rasilimali za umma ,ikiwemo upendeleo ,matumizi binafsi Katika Utumishi ,hali hiyo imedidimiza kufikiwa kwa lengo la Utumishi wa umma hivyo akawataka maafisarasilimaliwatu kujitathimini na mtumishi akikiuka achukuluwe hatua papo hapo na sio kuhamishwa.
Alisema kulingana na utafiti uliofanywa na Wizara umebaini kuna maeneo Maafisa raslimali watu hawatekelezi majukumu yao kulingana na viapo vyao ambavyo vinawwawezesha kuwa na Utumishi uliotukuka ili kufikia malengo ya taasisi zao
Alisema Kuna maeneo ya Sera,kanuni,Maadili na miongozo usimamizi unalegalega ,huo sio utendaji unaoridhisha kwa kuwa wengi hawawajibiki ipasavyo na kutahadharisha kwamba eneo litakalobainika lina mapungufu Serikali haitasitaa kuwachukulia hatua hivyo kabla hawakachukukuwa hatua wakatekeleze majukumu yao ipasavyo .
Alisema kuwa ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko ya watumishi Wastaafu hivyo akawataka maafisarasilimali watu wawe wanakaa na watumishi wanaokaribia kustaafu Ili kuwapatia elimu wawaandae vizuri,wawasilishe michango yao mapema Ili wanapostaafu wasisumbike ,wasiteseke na hatimae kufariki mapema wakihangaika mafao yao.
Aliwataka waache mtindo wa watumishi kukaimishwa kwa muda mrefu badala yake wafanye mchakato wa haraka wa kupata watumishi wenye sifa kujaza nafasi zinazobakia wazi ,kwa kuwa Maafisa rasilimali watu wamekuwa ni kikwazo .
Alikemea Utaratibu mbovu wa kila mkuu wa taasisi au Shirika kuchagua watumishi awatakao na kueleza kwamba hawana nafasi hiyo na Serikali itapanga watumishi kulingana na mahitaji hakuna mwenye mamlaka ya kuchagua watumishi awatakao huko ni kuvuruga mfumo mzima wa Utumishi wa umma na kuleta uanaharakati .
Awali kaimu Katibu mkuu Wizara hiyo,Xavier Daudi,alisema kuwa kikao hicho ni namna bora ya kukutana na kubadilisha mbinu za utumishi wa umma kwa lengo la kuendelea kuboresha Utumishi
Alisema bado kuna changamoto za masuala ya kiutendaji na Utumishi wa umma bila kuzingatia taratibu ,hali hiyo husababisha ucheleweshwaji wa huduma kwa wananchi hivyo kikao hicho kitajikita kutatua changamoto ambazo wamezibaini lengo ni kuboresha utendaji na huduma Katika Utumishi wa umma.
Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongela,alisema kuwa eneo la Utumishi wa umma ndio kwenye dhamana ya Utumishi na ndilo tegemeo la Viongozi,watumishi na wananchi kutokana na kusimamia mifumo ya Utumishi hivyo wataendelea kutoa ushirikiano ili kufikia malengo wanayoyatarajiwa.
Kikao kazi hicho cha Wakuu wa Idara za Utawala na rasilimali watu Katika Utumishi wa umma kimeandaliwa na ofisi ya Rais,manegmenti ya Utumishi wa umma na utawala bora kauli mbiu yake inasema Usimamizi wa raslimali watu unaozingatia maadili,Sheria na uwajibikaji na matumizi ya tehama ni msingi wa huduma bora Katika Utumishi wa umma.
Mwisho .