Site icon A24TV News

WAZIRI WA UTUMISHI NA UTAWALA BORA ZANZIBAR ASISITIZA UWAJIBAKI KATIKA OFISI ZA UMMA

Na Geofrey Stephen Arusha

WAKUU wa Idara za Utawala na Rasilimali watu Katika Utumishi wa Umma, wameelezwa  Moja wapo ya sifa ya Utumishi uliotukuka ni kujifunza na kusikiliza changamoto za watumishi waliopo chini yao na kuzitatua badala ya kukumbilia kufanya mabadiliko makubwa  ya haraka kwenye taasisi walizopangiwa au kuhamishwa.

Hayo yameelezwa Oktoba 13 na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Katiba na Sheria Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Haroun Ali Suleimani,alipokuwa akifunga kikao kazi kilichodumu kwa  siku tatu kwenye Ukumbi wa mikutano ya kimataifa,AICC Jijini Arusha.

Watumishi wanapewa vyeo watambue kuwa wameongezewa majukumu na sio upendeleo.

Amesema kwanza Maafisa hao wanatakiwa kujitambua wao ni nani Katika dhamana yao waliyonayo Katika kutoa huduma kwa umma.

Amesema moja wapo ya sifa iliyotukuka ya Utumishi ni pomoja na kutokufanya mabadiliko ya haraka wanapopewa majukumu kwanza wajifunze ,wasikilize watumishi waliopo na waache tabia ya kukaripia karipia haifai badala yake wazingatie maadili.

Amesema Utumishi wa umma una mambo manne ambayo ni Uzalendo,ambapo lazima wawe watiifu Kwa nchi ,wenzao Kwa kuwa cheo sio zawadi bali ni majukumu wawe na lugha ya upole.

Uwajibikaji watekeleze wasimamie wajitume na sifa meza zao kujaza mafaili huo ni uvivu katika maeneo ya kazi .

Jambo lingine ni Uaminifu,pamoja na kuacha matumizi mabaya ya fedha za umma.

Jambo lingine ni Usimamizi ,amewataka wasiamini waliopo chini yao Kwa asilimia 100 ,ambapo amesisitiza  wazungumze na watumishi wawasikilize matatizo yao na kero zilizopo wazipatie ufumbuzi.

Kauli mbiu ya kikao hicho inasema Usimamizi wa raslimali watu unaozingatia maadili ,Sheria,uwajibikaji na matumizi ya Tehama, ni msingi wa utoaji huduma bora Katika Utumishi wa umma.

Mwisho .