Site icon A24TV News

ZAIDI YA MIGODI 350 YA WACHIMBAJI WADOGO IMEUNGANISHIWA NA UMEME WA GIRIDI YA TAIFA DKT.BITEKO

Na Richard Mrusha

SERIKALI imesema kuwa inaendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwa pamoja na upatikanaji wa umeme wa uhakika pamoja na ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji ili kuharakisha ukuwaji uchumi.

Imesema kuwa hadi sasa baadhi ya migodi mikubwa ikiwemo Geita Gold Mines Limited (GGML) na STAMIGOLD Biharamulo Mine ambayo ilikuwa haina umeme kwa muda mrefu sasa imeunganishwa na umeme wa gridi ya Taifa

Akisoma hotuba hiyo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alitakiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kongamano la madini la kimataifa lililofanyika Jijini Dar es Salaam Leo Octoba 23 mwaka huu Naibu waziri mkuu DKT.Doto Biteko Amesema serikali imejipanga kuweka mazingira wezeshi Kwa wadau sekta ya madini.

Amesema migodi zaidi ya 350 ya wachimbaji wadogo imeunganishwa na umeme wa gridi ya Taifa na hivyo kupunguza gharama za uzalishaji na kurahisisha shughuli mbalimbali za migodi nakwamba Serikali inafahamu kuwa bado kuna mahitaji makubwa ya migodi kuunganishwa na umeme wa gridi ya Taifa

Amesema kuwa Sambamba na hilo, Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya usafirishaji ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa na barabara zinazounganisha maeneo yenye migodi na shughuli mbalimbali za madini ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa zinazoingia na kutoka migodini.

Kwa mfano “kwa sasa Serikali inaendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa barabara kutoka kijiji cha Paradiso hadi Kitai Mkoani Ruvuma yenye urefu wa kilomita 22 kwa kiwango cha lami na barabara ya Kabulo-Kiwira yenye urefu wa kilomita 7 mkoani Songwe kwa kiwango cha changarawe.”Amesema Naibu waziri mkuu Biteko

Nakuongeza kuwa “barabara hizo zitakapokamilika zitarahisisha usafirishaji wa makaa ya mawe kutoka migodini kwenda kwa watumiaji wa ndani na nje ya nchi.Ndugu Washiriki,Serikali inatambua na kuthamini mchango wa wachimbaji wadogo nchini katika kutoa ajira, kuboresha kipato kwa mtu mmoja mmoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.

Amefafanua kuwa kwa kutambua hilo, Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuwezesha shughuli za uchimbaji mdogo kufanyika kwa tija ikiwa ni pamoja na kununua mitambo mitano (5) ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo.

“Mitambo hiyo itawasaidia wachimbaji wadogo kufanya uchorongaji nakupata taarifa za uwepo wa mashapo ya madini kwa gharama nafuu Hivyo, napenda kuwafahamisha kuwa, Serikali imejipanga kuhakikisha Mashirika yetu mawili STAMICO na GST yanashirikiana kuwezesha upatikanaji wa taarifa za mashapo na hivyo wachimbaji wadogo kuboresha na kuongeza tija kwenye shughuli za uchimbaji madini hapa nchini. “Amesema

“Niwaombe kutoa ushirikiano wenu ili Serikali iweze kufanya kazi yake na kuwapatia taarifa sahihi za uwekezaji kwenye sekta hii ya wachimbaji wadogo,Ndugu Washiriki,Taarifa za kijiolojia watakazopata wachimbaji wadogo zitawawezesha kufahamu mashapo yaliyopo na kuongeza uzalishaji na hivyo kufanya uchimbaji mdogo kuwa wenye tija.”amesisitiza

Amesema kuwa taarifa hizo zitawezesha wachimbaji wadogo kukopesheka na hivyo kutatua changamoto ya upatikanaji wa mitaji. Nafahamu kuwa, mitambo hiyo ni michache, Serikali itaendelea kuongeza mitambo kadri fedha zitakavyopatikana.

“Niwahakikishie kuwa, mazingira ya uwekezaji katika Sekta ya Madini yameendelea kuboreshwa na kuwa rafiki zaidi,Nafurahi kusema kuwa, hadi sasa jumla ya Kampuni tisa (9) za Kimataifa za uchimbaji mkubwa wa madini zimeingia ubia na Serikali katika uchimbaji wa madini mbalimbali ikiwemo madini ya nikeli, kinywe, heavy mineral sands (mchanga bahari), Rare Earth Elements, dhahabu na almasi.

Hivyo, nitoe wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza zaidi Tanzania katika shughuli za utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji, uongezaji thamani na biashara ya madini. Serikali itaendelea kushirikiana na wawekezaji wa ndani na nje kwa manufaa ya pande zote mbili (win – win situation).

Nimefahamishwa kuwa baada ya kufunguliwa kwa mkutano huu kutakuwa na mada mbalimbali zitakazojadiliwa na wataalamu pamoja na wadau kutoka ndani na nje ya nchi,Nimeona mada zinazohusu madini muhimu na madini ya kimkakati (critical and strategic minerals), mada ya masuala ya utunzaji mazingira.

Mada hizi ni muhimu kutokana na muelekeo wa dunia wa kutaka kupunguza hewa ya ukaa kutokana na matumizi ya mafuta ya diseli na petrol kwenye magari. Niwaombe mtumie fursa ya mkutano huu kujadili na kupendekeza namna bora itakayotuwezesha kufungua milango ya uwekezaji kwenye hazina ya madini yaliyopo Tanzania kwa manufaa ya kiuchumi na kijamii pamoja na wawekezaji.

Serikali ipo tayari kupokea ushauri na mapendekezo yenu na kuyafanyia kazi kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Aidha, kwa masuala ambayo yatahitaji utekelezaji wa sekta binafsi, niwaombe muwe tayari kuyafanyia kazi ipasavyo ili kwa pamoja tuweze kufikia malengo tunayokusudia.

“kabla ya kumaliza napenda kuwakaribisha na kuwaalika kutembelea vivutio vya utalii katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu ikiwa ni pamoja na mbuga maarufu za wanyama za Serengeti na Ngorongoro pamoja na Mlima Kilimanjaro ambao mnafahamu kuwa ni mlima mrefu zaidi barani Afrika, bila kusahau fukwe nzuri za bahari, Zanzibar

.mwisho