Site icon A24TV News

Bunge la Afrika Mashariki lajadili maboresho ya kanuni pamoja na miongozo na sheria za uendeshaji .

Geofrey Stephen ,Arusha .

Arusha .Bunge la Afrika Mashariki EALA limejadili maboresho ya kanuni  ikiwemo miongozo na sheria za uendeshaji wake utakaosaidia kuongeza ufanisi wa shughuli zake katika utendaji kazi wa kila siku.

Akiongea mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa kwanza wa kikao cha pili cha bunge la tano la EALA Jijini Arusha, Mbunge wa Bunge hilo kutoka nchini  Kenya kennedy Kalonzo Musyoka  amesema kuwa yapo yaliyojadiliwa ambayo mengine hawajakubaliana nayo.

Kwa mujibu wa Musyoka amesema yale ambayo hawajakubaliana ikiwemo kuwepo kwa Naibu spika itapelekea kupiga kura ili kuweza kuyapitia au kutopitisha hivyo suala hilo litangojea uwepo huo.

“Tumekuwa katika kikao cha leo tukijadili marekebisho ya kanuni Miongozo na sheria za uendeshaji wa Bunge la EALA yapo tuliokubaliana na mengine hatujakubaliana mfano suala la kuwa na msaidizi wa spika hilo halijapita hadi sasa hivi  hadi tutakapopiga kura”amesema .

Hata hivyo kwa muda mrefu tumekuwa na changamoto ya Mawaziri kutohudhuria vikao kwani wengi wao hawaji kabisa na wanakuwa na shughuli nyingi  za serikali  na hali hii inachangia na kusababisha shughuli za  Bunge  kuzorota hivyo tunaomba wajitahidi kuja tusaidiane katika hii Kazi ya Jumuiya na kuhakikisha tunaharakisha shughuli za maendeleo katika jumuiya  yetu.

Kwa Upande wake Mbunge wa Bunge hilo kutoka Kenya David Ole Sankok amezitaka nchi za EAC kujenga ushirikiano katika Mtangamano wa forodha ya pamoja kwa kutembeleana bila kuwa na mipaka sababu hii mipaka iliwekwa na wakoloni.

Alisema suala la mtangamano wa Sarafu ya pamoja lakini viwango vya fedha zetu havilingani katika nchi zetu saba kwani  Kuna fedha ipo na nguvu na nyingine ipo chini kidogo lazima tuweze kuzilinganisha ndio tuwe na  shilingi  moja ya jumuiya ifikapo mwaka 2031 lakini kabla ya kufika huko tunatarajia tuanze kwa kutumia fedha zetu za ndani kwa biashara zetu za nchi za Jumuiya.

“Kwa sababu hakuna haja ya Mruwanda kubadilisha faranga kwa Dola ya Kimarekani ndio afanye biashara Tanzania kwani akifika Tanzania itambidi abadilishe Dola kwa fedha ya Tanzania hii ni kupoteza fedha nyingi sawa na asilimia 10 tunapoteza fedha nyingi baada ya Makato kwa biashara tulionayo baina ya nchi zetu sawa na bilioni 71 za kimarekani ukitoa asilimia 10 ya fedha hiyo ni ni nyingi kuliko bajeti zetu”

Aidha alitaka kuwepo kwa soko moja  ambalo ukiuza bidhaa za mipakani hakuna haja ya kubadilisha fedha zetu kwa Dola ya Kimarekani kwani watu  wengi  wanaofanya biashara ni wajasiriamali wadogo, wakulima, wafugaji na wengine hawajasoma ukiwaambia wabadilishe pesa kwa fedha za nje kabla hawajavuka mpaka itakuwa ni vigumu kufanya biashara tunataka kuwawezesha kufanya biashara bila kukabiliana na changamoto na changamoto yoyote.

 

Mwisho.