Site icon A24TV News

KIWAMADOLU WAIOMBA TUME YA MADINI KUWAONGEZEA MDA ILI WALIPIE LESENI ZAO 11.

Na Richard Mrusha, Mahenge

WACHIMBAJI wadogo wadogo wa kikundi cha KIWAMADOLU kinachojihusisha na uchimbaji wa madini ya Spinel kutoka mgodi wa Lukande uliopo katika Halmashauri ya ulanga mkoa wa Morogoro wameiomba Serikali kupitia Tume ya Madini kuwaongezea mda ili waweze kulipia leseni zao 11 ambazo mda wake umekwisha kwa kufanya hivyo wataweza kuchimba kisheria.

Wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya yakutembelea katika mgodi huo Mwenyekiti wa umoja huo wa KIWAMADOLU Ibrahim Manyerere amesema kuwa pamoja na kuendelea na uchimbaji mdogo mdogo katika mgodi huo lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo fedha zakuchukulia leseni zao ambazo tayari zina usajiri na namba isipokuwa kinachowakwamisha ni ifedha zakuchulia ila wakishapata fedha hizo ambazo ni kiasi cha shilingi milioni 13 wataendelea na uchimbaji

 

Aidha Manyerere ametaja changamoto nyingine ni kutokuwa na nyenzo za kisasa za uchimbaji ambapo wanatumia vifaa duni ambapo wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. Samia Suluhu Hassan kuwakumbuka wachimbaji wadogo wadogo kwakuwatafutia wawekezaji ambao watasaidia vifaa vya uchimbaji kwa kufanya hivyo itawasaidia kupata uzalishaji wa tija

“Kwanza kabisa shukurani zetu za pekee kwa mkuu wetu wa Wilaya amekuwa akitupa ushirikiano yeye ndie amesababiaha sura hizi zinaonekana hapa kwa malezi yake na ushauri kwetu imani kubwa na Waziri pili tunamshukuru waziri wetu wa madini Antony Mavunde anafanya kazi nzuri yakuhamasisha hata wawekezaji wa madini wakubwa kuja nchini kuwekeza katika sekta ya madini hivyo mbali na ombi la leseni tunaomba pia atafute muda aje kusikiliza kero zetu zile zenye kutolewa ufumbuzi kwa haraka na zile za maelekezo tupo tayari kufuata.”amesema Manyerere.

Naye Elizabeth Kurwa ambae ni mmoja wa wachimbaji wadogo wadogo wanawake amesema uchimbaji wao bado ni duni na pesa wanayopata haiwatoshelezi kulipia deni ambalo wanadaiwa kwa ajili ya kulipia leseni zao hivyo wameomba mamlaka husika kuwaangalia kwa jicho la tatu kuweza kulejeshewa leseni zao.

Ameongeza kuwa wanaiomba serikali kuwaunganisha hata na Taasisi zakifedha ili kuwapatia mikopo kwa lengo la kupata mitaji na kuweza kununua vifaa vya kisasa vya uchimbaji ili wachimbe kisasa na kuweza kupata kipato.

Kwa upande wake Ben Mpenda ambae ni Makamu Mwenyekiti amesema mpaka sasa wana jumla ya wanachama 581 waliowasajiri pamoja na kuweka mipango mbalimbali ya maendeleo na mipango ya faida katika maeneo hayo ikiwemo mwekezaji anatakiwa kufuata katiba ya kikundi chao kwakuweka asilimia 30 katika kikundi chao ili wanakikundi kuweza kunufaika na uwekezaji.

“Eneo hili linapatikana madini aina tano tofauti ikiwemo Spinel ambapo thamani yake ni kubwa inataka kulingana na thamani ya madini ya Almas ila changamoto ni nyenzo kwa sasa tunachimba kwakutumia sululu na chepe hivyo endapo tukipatiwa nyenzo za kisasa na elimu ya uchimbaji itatusaidia kuchimba kisasa ambapo tutajikwamua kiuchumi na kuchangia pato la taifa .
“Amesema Ben:

Mwisho