Site icon A24TV News

Prof Mkenda, UNICEF wajadili namna bora ya kutekeleza Sera ya Urejeshaji shuleni wanafunzi waliokatisha masomo

Na Mwandishi wa A24tv Dodoma .

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda leo Novemba 8, 2023 Jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Timu ya Ujumbe wa UNICEF ukiongozwa na Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Bi Eike Wisch.

Katika mazungumzo hayo viongozi hao wamejadili kuhusu Sera ya urudishwaji wa wanafunzi waliokatizwa masomo kutokana na sababu mbalimbali kama vile utoro, utovu wa nidhamu, kupata ujauzito na walioshindwa kuhudhuria masomo kwa muda mrefu.

Wamesema uamuzi huo wa kuwarejesha shuleni wanafunzi hao umewapa fursa kupata elimu ambayo ni haki ya msingi na kuwasaidia kukamilisha mzunguko wa elimu katika mfumo rasmi wa elimu.

Aidha, viongozi hao wamejadili namna bora ya utekelezaji wa Sera hiyo ikiwa ni pamoja na kuwezesha tafiti mbalimbali za kubaini na kuendeleza afua zenye kujielekeza katika kupunguza tatizo la mdondoko wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na ujauzito kwa wanafunzi wa kike.

Mwisho