Site icon A24TV News

TAMASHA LA WANAWAKE NA UTALII (FESTIVAL)RASMI KUZINDULIWA TEREH 17 NOVEMBA 2023 NA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII ARUSHA .

Na Geofrey Stephen Arusha .

Tamasha kubwa la kihistoria la wanawake festival kutikisa viunga vya jiji la Arusha na Mkoa kwa ujumla ambapo Waziri wa Mali asili na utalii Anjela Kairuki anatarajiwa kufungua tamasha la hilo la aina yake la  Wanawake festival litakalofanyika November 17 jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa Simba hall  Aicc.

Tamasha linalenga kuwezesha kufikia idadi ya watalii milioni Tano ifikapo mwaka 2025

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha mwenyekiti wa tamasha hilo Nengasu Werema amesema kuwa wameamua kuunga serikali mkono katika jitiada za kutangaza utalii.

Alisema kuwa wao kama wanawake watafanya tamasha hilo ambalo litashirikisha wanawake na wadau wa utalii kwa pamoja ili Wanawake waweze kushiriki kwenye sekta ya utalii.

“Tunataka kutangaza na kukuza sekta ya utalii kwani mada kubwa ya festival hii ni kuangalia namna ambavyo Wanawake wanaweza kujihusisha katika sekta ya utalii ambayo itawezesha kukua kwa uchumi wa Tanzania na wa mtu mmoja mmoja”aliongeza

katika tamasha hilo kutakuwa na tuzo mbali mbali ambazo zitatolewa kwa Wanawake vinara wa utalii lakini pia wataweza kutembekea vivutio vya utalii ikiwemo ya hifadhi ya taifa ngorongoro na na hifadhi ya tarangire.

Kwa upande wake afisa uhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa tarangire Jully Bede aliwapongeza Wanawake hao kwa kuandaa tamasha hilo na kuhaidi kuwapa ushirikiano ikiwemo kuwaeleza Wanawake fursa zilizopo kwenye hifadhi.

Naye mkurugenzi wa Wanawake na utalii Mercy Michae alisema kuwa lengo la wao kuandaa tamasha hilo ambalo litashirikisha wanawake walioko kwenye sekta ya utalii ni kuhamasisha Wanawake kuunga mkono sekta ya utalii kuwekeza katika sekta hiyo na hatimae kuweza kuongeza pato la taifa.

Mwisho