Site icon A24TV News

VIGOGO,NA WAFANYA BIASHARA WAKUBWA ARUSHA WAPIGANA VIKUMBO KUCHUKUA FOMU YA NAFASI YA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA ARUSHA

Na Mwandishi wa A24tv Arusha

Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Arusha kimefungua pazia kwa wanachama wake   kuziba nafasi ya mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti wake ZELOTHE STEVEN ZELOTHE baada ya kufariki  Oktoba 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akiongea na vyombo vya habari katibu wa CCM mkoani Arusha Musa Matoroka alisema kuwa nafasi hiyo kwa sasa ipo wazi na wanachama wa ccm wanapaswa kuchukua fomu zilizoanza kutolewa leo makao makuu ya chama hicho mkoani Arusha kwa ajili ya mchakato wa kuziba pengo hilo. 
“Kuanzia jana tarehe 21 fomu za kuwania nafasi ya mwenyekiti wa ccm zimeanza kutolewa hadi siku ya Alhamis saa kumi kamili jioni na mwitikio ni mkubwa na wanachama wanajitokeza” 
Aidha aliongeza kuwa fomu za kuwania nafasi hiyo zinatolewa bure kwa wanachama mwenye sifa ndio wanaopatwa kujitokeza na kuchukua fomu hizo.
Matoroka aliwataka wanachama hao kuzingatia utaratibu wa chama hicho kwa kutojihusisha na kampeni za kuchafuana au kutoa rushwa kwani kwa kufanya hivyo ni kukiuka taratibu za chama na jina litaondolewa.
Alisema hadi Leo majira ya mchana wanachama zaidi ya 20 wa ccm walikuwa wamejitokeza kuchukua fomu na miongoni mwao ni pamoja na ,aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Morogoro Erasto ole Sanare pamoja na mwanasiasa Mkongwe Musa Mkanga na dkt Daniel Palangyo aliyewahi kuwa Mnec Arusha
Zoezi hilo linatarajiwa kufungwa siku ya alhamis saa 10 jioni kuchukua fomu na kurejesha .
Mpaka sasa vigogo wakubwa ambao ni makada wa chama chapinduzi wamesha chukua fomu za kugombea nafasi hiyo kubwa katika mkoa wa arusha wakiwemo pia wafanya biashara wenye majina makubwa na eshma katika chama chamapinduzi Ccm .
Mwisho