Site icon A24TV News

ZARA TOURS YAZINDUA TWENZETU KILELENI ,RC BABU AMPONGEZA MKURUGENZI KWA KUJALI MAZINGIRA

Na Geofrey Stephen , Kilimanjaro.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe Nurduni Babu amewataka watanzania kujitokeza Kwa wingi katika zoezi la upandaji mlima Kilimanjaro linaloenda sambamba na kusherehekea miaka 62 ya uhuru wa nchi ya Tanzania.

Pichani ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu pamoja na uongozi wa kampuni ya Zara tour Killmanjaro sambamba na wadau wengine wa kiserkali mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya Twende Zetu Kileleni tarehe 5/12/23

Ameyasema wakati wa zoezi la  uzinduzi wa kampeni ya Twende Zetu Kileleni mlima Kilimanjaro iliyoandaliwa kampuni ya Zara Tours  ya mkoani Kilimanjaro.
Alisema kuwa kampeni hiyo siyo ya kwanza kufanyika,ambapo zaidi yawatanzania 320 wanatarajiwa kushiriki ambapo katika kampuni ya Zara watapanda watu 200 na kmapuni zingine 70 na zingine 50 hivyo hiyo ni maendeleo makubwa ya kampeni hiyo ya Twende Zetu Kileleni.

Alitumia nafasi hiyo kumpongeza mkurugenzi wa Zara tour kuhamasisha upandaji wa mlima Kilimanjaro pamoja na kuwa kipaumbele katika kutatua changamoto pindi zinapojitikezakatika mlima Kilimanjaro.

 filamu ya The Royal Tour iliyozinduliwa na Daktari Samia Suluhu Hassan imeleta mafanikio makubwa katika nchi ya Tanzania na sekta hiyo Sasa Iko mbele ikizidi kufanya vizuri.
Pamoja na hayo mkuu wa mkoa Babu amesema kuwa katika kuimarisha utalii na kuwapa huduma watalii pindi wanapokuwa na changamoto mbalimbali Zara tour Kwa kushirikiana na kampuni ya Kill media wamehakikisha usalama wa watalii.
Alitoa rai kwa watanzania kupanda mlima wa Kilimanjaro  na kuhakikisha wanajitokeza Kwa wingi kwani viongozi nao watakuwa msitari wa mbele kupandalima huo.
Alisema kuwa  serikali ya mkoa imedhamiria kurudisha kijani ya mkoa wa Kilimanjaro Kwa  kutekeleza zoezi la upandaji mti  kufuatia Sasa barafu eneo la  mlima Kilimanjaro kupungua  hivyo kampeni hii ya kupanda mlima iende sambamba na kupanda miti eneo hilo.
Naye Mhifadhi shirika la hifadhi Tanzania Gladyness  Ng’umbi  alisema kuwa zoezi la kupanda mlima lilianzishwa na Hayati  Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania awamu ya kwanza Mwalimu Julius Nyerere 
Alisema kuwa watanzania wanapaswa kufahamu kuwa vivutio vilivyopo Tanzania ni Kwa ajili yao na si Kwa ajili ya wageni tu ambapo katika zoezi la upandaji mlima mwaka huu ladha ya kupanda mlima imeongezwa Kwa kupitia geti la Machame,kibosho na marango ili kujionea zaidi vivutio.
Alisema kuwa wao kama hifadhi ya Taifa Kwa kushirikiana na kampuni za kitalii wamejipanga  ipasavyo  hivyo watanzania watakaopanda mlima Kilimanjaro wamehakikishiwa viwango vya ubora vya kupanda mlima
Kwa upande wake  mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Zara Tour Bi Zainab Ansell amesema kuwa kampuni ya Zara your itaadhimisha miaka 62 ya uhuru Kwa kupanda mlima Kilimanjaro tarehe 5/12/2023.

Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya utalii ya  Zara tour Bi Zainab  Ansell

Kampuni ya Zara Tour imempongeza Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kutangaza sekta ya utalii ipasavyo ambapo kampuni hiyo Sasa imeendelea kuenzi  sekta hiyo  utalii  nchini ambapo sasa imekuja na  Kampeni ya Twende Zetu Kileleni mlima Kilimanjaro lengo ni kuhamasisha utalii wa upandaji mlima Kilimanjaro pamoja na kusherehekea miaka 62 ya uhuru.
Alisema kuwa zoezi hilo limeshirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya utalii ndani na nje  ya nchi ya Tanzania na lengo ni kuendelea kutangaza vivutio vilivyopo katika mlima Kilimanjaro na sekta ya utalii Kwa ujumla.
Pamoja na hayo kampuni ya Zara tour imesema kuwa inakuletea msimu wa tatu ambapo tarehe za safari ni kama ifuatavyo siku ya kwanza ni ya kuwasili Moshi Kilimanjaro,na siku ya kwanza Hadi ya nane katika siku ya kupanda mlima Kilimanjaro ni tarehe 5,6,7,8,9,na 10 Des
Gharama za kushiriki katika zoezi Hilo la kupanda mlima ni shilingi 1,150,000 Kwa Kila mtu ambapo gharama hizo zitahusisha  vifaa na chakula,usafiri wa kwenda Marangu Gate pamoja na Tozo zote za serikali zitakazohusisha  na safari  hiyo 
Siku ya mwisho  itakuwa siku ya Kurejea nyumbani baada ya safari ya kupanda mlima
Watu wote mnakaribishwa  kwenda kupanda mlima Kilimanjaro.