Na Geofrey Stephen Arusha.
Wahitimu wa Taaluma mbalimbali nchini wameshauriwa kutowekeza katika maarifa ya darasani Pekee kwenye kutekeleza majukumu yao badala yake kuwa na utashi utakao wawezesha kubadili mitazamo hasi ya Jamii na hivyo kutokuwa chanzo Cha mitafaruku katika maeneonyao ya kazi .
Hayo yamebainishwa katika mahafali ya Saba ya Chuo kikuu Cha Mtakatifu Agustino Tawi la Arusha. Ambapo Askofu wa Jimbo kuu katoliki la Singida EDWARD MAPUNDA Akiwatunuku Astashahada, Stashahada na Shahada ambao wanafunzi wa fani mbali mbali chuoni hapo.
Amesema kwamba wanafunzi walio pata elimu chuoni hapo wanapaswa kuepuka athari zitokanazo na kasumba ya waajiri na wanataaluma kuzingatia elimu ya darasani Pekee na kushindwa kuakisi uwezo wa waajiriwa Kwa kumudu hisia zao katika kufanya maamuzi.
Kw upande wake Mkuu wa chuo kikuu Cha Mtakatifu Agustino Tawi la Arusha Dkt. Charles Rufyariza ametoa rai Kwa hitimu kutendewa kazi Kwa weledi Yale waliyojifunza Kwa miaka mitatu ya mafunzo Yao.
Amesema angependa kuona wanagunzhi hao wamkua mfano mkubwa wa kuivwa katika kutimiza majukumubyao ya kazi kwa uweli nankua mfano katika tahasisi watakazo tumimia na sio kikwazo kwa jamii inayo wazunguka kwani wamefundishwa vyema namna ya kuwaeshimu watumishi pamoja na jamii watakao tumikia2
Nao wahitimu wa ngazi mbalimbali wanaeleza namna kukosekana Kwa taaluma kumechochea kudidimiza Taasisi na Sekta mbalimbali,na kubainisha kuwa ni wajibu wa Taaluma kuchukua nafasi yake Ili kuwepo na mabadiliko chanya na ya Haraka kwenye jamii.
Wahitimu hao wameshukuru Mh Rais kwa kuwapa fursa ya kupata mikopo kwa asilimia 100 bila usumbufu wowote jambo ambalo limewasaidia katika kuzingatia masomo pasipo na usumbufu wa kurejea nyumbani kutafuta fedha za kujikimu katika masomo yao.
Wahitimu hao wameitimu.katika kozi mbali mbali ikiwemo shahada ya uzamili katika utawala bora wa elimu sayansi , Stashahada ya utawala na biashara , Stashahada ya uhasibu ,Astashahada ya uhasibu ,Stashahada ya sheria ,na Astashahada ya sheria Stashahada ya Elumu na Sayansi Stashahada ya kwanza ya Utalii na Ukarimu
MWISHO.