Na Ahmed Mahmoud
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha kimepongeza waandaaji wa mbio za Mount Meru Marathon Kwa kujitolea vifaa mbalimbali kusaidia Uzazi Salama kwa wakinamama wasio na uwezo wa kununua vifaa vya kujifungulia.
Akiongea Mara baada ya kuwakabidhi vifaa hivyo katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru na kuzindua Bonanza hilo la kesho katika viwanja vya Ngarenaro Katibu wa itikadi na Uenezi Mkoa wa Arusha Saipulan Ramsey Jijini Arusha amesema Mount Meru Marathon imeonyesha kuunga Ilani ya CCM.
Amesema katika Ilani yao ukurasa wa Tano inaeleza kuimarisha huduma za mama na mtoto na niwapingeze kwa kugusa ibara ya 8 ukurasa 5 ikiwemo mazingira mazuri ya mtoto kuja Duniani mlichokifanya Leo ili kuongeza idadi ya watu.
“Serikali pekee haiwezi kufanya kila kitu ila ni kuwapa na kuwafunguli fursa wadau wa maendeleo ambao wapo teyari kuunga juhudi za utekelezaji wa ilani ya chama chetu au juhudi za uimarishaji wa Afya ya mama na mtoto hivyo nitumia fursa hii kuwaomba wadau wengine kujitokeza na kujitolea katika suala hili ya Afya salama”
Kwa Upande wake Mwanzilishi wa Mount Meru Marathon Sports Promotion Dinnah Mushi amesema Lengo la bonanza hilo ni kuwanyanyua vijana wote nchini kuona jinsi gani wanavyoweza kujitambua pamoja na kusaidia mama anayejifungua na vifaa vyote vikiwa salama.
Awali akiongea Afisa ustawi wa Jamii hospitali ya Mount Meru Teresia Constantine amewashukuru sana Mount Meru kwa vifaa hivyo akieleza vitatumika kwa wagonjwa watakaojifungua Leo na vitakavyobakia watavitumia kwa kinamama wengine.
Nae Meneja wa Tawi wa Benki ya KCB Oprah James ambao ndio wadhamini wakubwa wa Mount Meru Marathon wameeleza kuguswa kwa tukio hilo la kutoa vifaa vya kujifungulia kwa kina mama kwao wakiwa kama wadau wa maendeleo wataendelea kujitolea kurudisha faida kwa Jamii.
Mwisho .