Site icon A24TV News

CEDB YAZINDUA KADI YA KISASA AMERICAN EXPRESS YA KAMPUNI KUBWA DUNIANI RC MONGELA APONGEZA

Na Geofrey  Stephen Arusha

Benki ya CRDB imezindua Matumizi ya Kadi ya American Express moja ya kampuni kubwa za huduma za malipo duniani katika mtandao wa Benki CRDB mkoani Arusha.

Akizindua Matumizi hayo Mkuu wa mkoa wa Arusha bw.John Mongela alisema kuwa mfumo wa malipo ni moyo wa uchumi wowote ule kote duniani na ufanisi wake ni muhimu kwa maendeleo endelevu.

Alisema kuwa Miundombinu imara ya malipo inarahisisha sio inawezesha kufanyika kwa miamala bali pia inachochea ukuaji wa kiuchumi, na inaongeza ujumuishi wa kiuchumi kwa Wananchi.

“Katika uchumi wa dunia ya leo unaoendelea haraka, ambapo teknolojia ya kidijitali imeshika hatamu, ushirikiano kama huu tunaoona leo kati ya Benki ya CRDB na American Express unachukua jukumu muhimu katika kuwezesha mustakabali mzuri wa mfumo wetu wa kifedha.”Alisema bw.Mongela

Pia alisema Ushirikiano huu baina ya Benki ya CRDB na American Express unaendana na maono ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ya kukuza biashara na utalii nchini Tanzania.

Kwa Upande wake Makamu mwenyekiti wa Bodi ya CRDB Profesa Neema Mori alisema kuwa ushirikiano huo utasaidia kukuza mapato na fedha za kigeni katika maeneo ya utalii hususan mkoa wa Arusha.

Pia aliongeza kuwa watalii wataweza kufanya malipo ya Serikali ikiwamo kulipia Visa na tozo nyingine stahili kwani mfumo tayari umeunganishwa moja kwa moja na mfumo wa malipo ya Serikali GePG.

Kwa Upande wake bi.Briana Wilsey, Makamu wa Rais, na Meneja Mkuu EMEA, Huduma za Mtandao wa Kibadilishanaji Kimataifa, American Express,Mpaka Sasa wanatoa huduma katika nchi 90 na kadi 130.

Bi.Briana alisema wameamua kushirikiana na CRDB Kwa kuwa ni benki inayokua kwa kasi ya hali ya juu,inatoa huduma nchi za maziwa makuu ambazo ni Tanzania ,Burundi na Congo,Mtandao mpana wa wadau na wananchama wake hivyo mashirikiano hayo yatataongeza mapato kupitia Sekta ya Utalii.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo bw.Abdulmajid Nsekela alisema kuwa CRDB ni benki ya kwanza ya kizalendo nchini kuingia Makubaliano na kampuni ya American Express ambapo italeta mapinduzi makubwa ya kiteknolojia kwenye sekta ya fedha ambapo ushirikiano huo sio tu utakwenda kuongeza ubora wa kutoa huduma kwa Watalii na wafanyabiashara,bali pia utawawezesha kufanya miamala yao kwa urahisi,iwe ni malipo ya huduma za malazi, chakula,na malipo mengine katika sehemu mbalimbali za huduma.

Alisema kuwa benki hiyo kiongozi ni ya kwanza nchini Kwa ubunifu wa bidhaa mbali mbali ikiwemo Tembo Kadi na Visa Kadi.

“Ushirikiano huu utaendelea kuimarisha zaidi Mapinduzi ya Kiuchumi nchini mfano katika mkoa huu wa Arusha ambao ni kitovu Cha Utalii wadau kama TANAPA, Ngorongoro, TATO na wengineo wataweza kunufaika na hudumu hii Kwa urahisi zaidi na tutaendelea kuwa wabunifu Ili kuweka mazingira mazuri na mepesi Kwa wateja”Alisema bw.Nsekela

Aidha kwa mwaka huu pekee (2023) taarifa za Fedha za benki ya CRDB zinaonyesha kuwa takribani miamala Milioni 4 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 300 imefanyika kupitia mfumo huu.

Hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Gran melia Jijini Arusha imehuduhuriwa na Wadau mbali mbali ambao wameonekana kufurahi huduma hiyo ya Kimataifa.
 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.John Mongela akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa Matumizi ya Kadi ya American Express moja ya kampuni kubwa za huduma za malipo duniani katika mtandao wa Benki CRDB mkoani Arusha.


Bi Briana Wilsey Makamu mwenyekiti wa Raisi na meneja mkuu EMEA,Huduma za Mtandao wa Kubadilishanaji Kimataifa AMERICAN EXPRESS akizindua akisubiria Risiti mara baada ya kufanya Malipo kupitia Huduma hiyo

Wadau Mbali mbali kutoka mkoani Arusha wakifuatialia Uzinduzi wa Huduma hiyo kutoka benki ya CRDB na kampuni ya AMERICAN EXPRESS katika hoteli ya Gran melia.

Mwisho