Site icon A24TV News

GARI JIPYA LA CRDB LAENDA KWA MKUU WA CHUO MAENDELEO YA JAMII ARUSHA.

Na Geofrey Stephen .
Benki ya CRDB imekabidhi gari jipya aina ya Vanguard lenye thamani ya Milioni 30 kwa mshindi wa jumla Dkt Bakati Zuberi akitokea Mkoani Arusha,aliyeshinda kupitia kampeni maalumu ya Benki ni SimBanking kupitia simu za mkononi.
Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi gari hilo ,iliyofanyika katika benki hiyo tawi la Usariver wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.
Mkuu wa Kitengo cha wateja na biashara ,Steven Adil alisema benki ya CRDB ilitenga kiasi cha sh,milioni 350 kwa ajili ya kampeni hiyo iliyozinduliwa februali 14 mwaka huu,Mbagala jijini Dar-Es-salaam.

“Kampeni hiyo imekuwa na manufaa makubwa sana kwa watanzania wenye kufahamu huduma zetu za kidigitali zinazopatikana benki ikiwemo mikopo na akaunti.

Mwisho.