Site icon A24TV News

MAKONDA AWAPA SIKU 10 WATUMISHI WA SERIKALI KUJITATHIMINI KWENYE NAFASI ZAO

Na Richard Mrusha

CHAMA cha Mapinduzi CCM kimetoa wito kwa watanzania kujitokeza kushiriki na kutoa maoni yao katika Dira ya Maendeleo ya taifa ya mwaka 2025 -2050 ili kuchagua Tanzania wanayoitaka.

Katibu Mwenezi wa CCM, Paul Makonda amebainisha hayo leo Desemba 21, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa Lengo la kuzungumzia ziara zilizofanywa na viongozi wao katika kuimalisha chama.

Pia amefafanua kuwa mchakato wa kutoa taarifa kwa vyombo vya habari utakuwa ukifanyika kila baada ya robo mwaka ili kutoa fursa kwa wanaccm na wananchi kufahamu yaliyotekelezwa,baada ya ziara za viongozi wao.

“Tunashukuru baada ya kufanya ziara katika mikoa mbalimbali nchini tija imeanza kuonekana baada ya waziri wetu wa Ardhi Nyumba na Makazi, Jerry Silaa amefanya kazi bora ambayo kwetu CCM ni ya kujivunia baada ya kutatua migogoro mkoani na Dodoma na kuwaondosha watendaji 15 waliobainika kuhusika na migogoro hiyo,” amsema.

Pia ameongeza kuwa mwaka huu unaofikia tamati siku chache zijazo watumishi wote wa Serikali wajitathimini kama wameweza kumsaidia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kiutendaji na ikifika Januari, 2024,wawe wamepata majibu ya kuamua kama wanafaha au la katika nafasi hizo.

Pia akizungumzia suala la kukatika kwa umeme mara kwa mara jambo ambalo limekuwa kero kwa watanzania, amesema kwamba suala hilo haliwafurahishi hata wao hali ambayo wanatafakari namna ya kuwabana watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) hata baada ya kuwaondosha viongozi wa juu pekee.

“,Kila wakati baada ya kutokea hadha ya umeme hatua zimekuwa zikichukuliwa kwa viongozi wa juu kuwajibishwa sasa umefika wakati katika vikao vyetu vya chama tuangalie namna ya utendaji wa wafanyakazi waliobaki ili kujua uwezo wao na ni vema wakaanza kujitathimini na kujua hatma yao mapema kabla hatujawafikia,” amesema.

Makonda amesisitiza kuwa ili kuendelea kukiimarisha chama, Januari 15, 2024 wataanza ziara katika mikoa 10 wakianzia Mkoa Pwani na kuendelea katika mikoa Tanga, Shinyanga, Tabora, Morogoro,Kilimanjaro, Manyara,Simu,Singida, Arusha na.
Katika ziara hiyo amewataka wananchi wenye kero mbalimbali kujitokeza kuzitoa na kuzipatia ufumbuzi ili wapate amani na utulivu katika maeneo yao.

Pia amewataka watendaji na watumishi wa umma katika maeneo ambayo ziara hiyo itapita kujipanga mapema katika kutatua kero za wananchi na ambaye bado hayuko sawasawa ajitathimini mapema.

MWISHO