Site icon A24TV News

NASSARI KUONGOZA UWEKAJI WA BIKON NA KUPIMA ARDHI KIJIJI CHA BWAWANI MONDULI

Na Geofrey Stephen ,Monduli

Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha,Joshua Nassari amesema ataongoza zoezi la upimaji wa Ardhi na kuweka bikon katika kijiji cha Bwawani Moita na kuakikisha wananchi wanaondokana na migogoro isiyo kua na tija na kushindwa kufanya kazi za maendeleo katika kata hiyo .

Nassari alisema hayo baada ya kuongea na viongozi wa Kijiji cha Moita Bwawani na kusema kuwa serikali inajua kila kitu juu ya mgogoro wa ardhi kwani baadhi ya viongozi wanajipanga na chaguzi zijazo hivyo wanashirikisha wananchi katika kujiandaa na uongozi miaka ijayo.

Akizungumza katika mikutano miwili tofauti ya hadhara ya wananchi wa Kijiji cha Moita Bwawani alisema ardhi ekari 7000 ni mali ya Kijiji cha Moita Bwawani hivyo viongozi na wananchi wa Kijiji hicho wanawajibu wa kupanga matumizi ya ardhi hiyo.

Mkuu huyo wa Wilaya alisema kila mwananchi anapaswa kushirikishwa katika maamuzi ya ardhi hiyo kwa maendeleo ya Kijiji na sio kutoa ardhi kwa ajili ya watu wachache wenye lengo la kujifaisha na kuacha wananchi wakiteseka.

Alisema jamii ya kifugaji ya kimasai inahitaji eneo la ardhi kwa ajili ya malisho na Kijiji kinahitaji sehemu ya ardhi hiyo kwa ajili ya makazi hivyo aliwataka viongozi kuangalia namna ya kutatua tatizo hilo kwa kupitia vikao husika vitakavyoshirikisha wananchi wote wa jamii hiyo ya kifugaji .

Pamoja na hayo aliwataka viongozi wote wa serikali ya Kijiji cha Moita Bwawani,diwani wa kata ya Moita Bwawani pamoja na mtendaji wa kata kufika ofisni kwake siku jumatatu desemba 18 mwaka huu kila mmoja akiwa na nyaraka zenye kuhalalisha mgogoro wa ardhi ekari 7000.

 

Naye Sanare Mollel maarufu kwa jina la Muller Mwananchi wa  alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kusitisha eneo hilo la ardhi kwa ajili ya makazi na kusema kuwa uamuzi huo umezingatia maslahi ya wafugaji wa kijiji cha Moita Bwawani

Muller alisema kutoa ardhi ya malisho kwa aajili ya makazi ni kutaka kuwaumiza wananchi wa Kijiji cha Moita Bwawani kwani wengi wao ni wafugaji na wanahitaji eneo hilo kwa ajili ya malisho kitu ambacho kutoa kuwa enel la makazi sio sawa kabisa.

Awali Mwenyekiti wa Kijiji cha Moita Bwawani,Bruno Mollel aliwataka wanachini wa Kijiji hicho kuacha jazba dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli kwani ardhi ekari 7000 iko ndani ya kijiji chao na wao ndio wenye uwezo wa kupanga matumizi ya ardhi hiyo na sio wananchi wa vijiji vingine.

Mollel alisema chokochoko zote za wananchi wa Kilimatinde na Moita zinachochewa na baadhi ya wanasiasa na watu wenye uwezo wa kifedha lakini maamuzi ya wengi yamezingatiwa na ndio maana serikali ilitoa hati ya ardhi hiyo na kuamua kumega eneo la malisho kwa ajili ya makazi.

Mollel alisema kuwa vikao vya kijiji na halmashauri ya Kijiji vilikaa na kupata Baraka ngazi ya wilaya hivyo wale baadhi ya wote  wanaopinga utoaji wa ardhi kwa ajili ya makazi hawana hoja za msingi kwa kuwa serikali ilishabariki na hatimaye kuridhia utoaji wa ardhi hiyo.

 

Mwisho