Site icon A24TV News

Serikali Kuendelea kulinda Viwanda nchini

Na Mwandishi wa A24tv.

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji Mb), amesema Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha viwanda vya wawekezaji wa ndani na nje vinalindwa ili viweze kuzalisha ajira kwa Watanzania.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Desemba 23, 2023 alipotembelea Kiwanda cha Kahawa cha Amir Hamza (T) Ltd kilichopo Mkoani Kagera ili kujionea shughuli za uzalishaji, kusikiliza na kutatua changamoto zinazokikabili kiwanda hicho.

“Viwanda vikizalisha bidha na vikapata faida, vitaongeza uzalishaji. Kadri kiwanda kinavyokua ndivyo kinavyohitaji malighafi na kuongeza ajira kwa Watanzania”. Amesema Dkt. Kijaji

Akiwa kiwandani hapo Dkt. Kijaji amebainisha kuwa Kiwanda hicho cha AMIZA chenye uwezo wa kuzaliha ajira za kudumu 400 na za muda 600 ni moja ya viwanda vinavyouza bidhaa zake kupitia soko la Eneo Huru la Biashara Afrika(AfCFTA)

Akiongea kuhusu changamoto zinazokikabili kiwanda hichi amebainisha kuwa Serikali inaendelea kujipanga na kuona namna ya kuwezesha viwanda kupata fedha za kutosha za kununua kahawa kutoka kwa wakulima(vyama vya msingi).

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kahawa cha Amir Hamza (T) Ltd, Bw. Amir Hamza amesema Kiwanda hicho kinauwezo wa kuchakata tani 72,000 ya kahawa ya maganda kwa mwaka na kinauza kahawa yake nchini na katika nchi za Uganda, Kenya, Marekani, India na nchi za Uarabuni

Mwisho.