Site icon A24TV News

Wananchi wa Kyela watakiwa kulima kilimo cha kakao kibiashara

Na Mwandishi wa A24tv .

Wananchi wa Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya wametakiwa kufanya kilimo biashara katika zao la kakao ili kuinua uchumi wao kutokana na zao hilo kuzidi kupanda bei.

Ushauri huo umetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Exaud Kigahe(Mb) Desemba 18,2023 wakati wa ziara yake ya kuona maendeleo ya zao la biashara la kakao wilayani Kyela.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Exaud Kigahe (Mb) akiangalia tunda la zao la Kakao katika Shamba darasa la Bw. Isaya Wilayani Kyela Desemba 18, 2023.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo amewataka Wizara ya Kilimo kupitia maafisa ugani kutoa elimu kwa wakulima ili kuzalisha kibiashara zaidi kwani zao hilo limekuwa na faida kubwa katika kuinua uchumi wao na Taifa kwa Ujumla.

Aidha Mhe Kigahe amezielekeza Taasisi za SIDO na TIRDO kufanya utafiti wa namna ya kuzalisha bidhaa ya ziada inayotokana na mbegu ya zao hiyo ikiwemo kuzalisha juisi na pombe ya kisasa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Ndg.Asangye Bangu akizungumza na Wakulima wa Zao la Kakao Wilaya Kyela juu ya Umuhimu wa kuweka Zao la kakao yebye ubora kwenye ghala.

Vilevile Mhe.Kigahe amesema kuwa ziara hiyo ina lengo la kuhakikisha Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara inaendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji wa biashara katika kilimo hususani wa zao hilo pamoja na kufurahishwa na mfumo wa stakabadhi ghalani na kupanda kwa bei ya zao la Kakao kutoka Sh 9,800 mpaka Sh10,000.

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Josephine Manase amewataka wananchi na wakulima wa zao hilo wilayani hapo kulilimda zao la kakao pamoja na kuacha tabia ya kuuza zao hilo kwa watu wakati badala yake wafike katika minada inayotangazwa ili kuuza zao hilo kwa bei elekezi inayotolewa.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Exaud Silaoneka Kigahe (Mb) akiwa ameambatana na
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw. Asangye Bangu na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase wakiangalia miti ya kakao katika shamba la Kakao la Bw. Isaya pamoja na kushiriki zoezi la mnada namba 25 wa Kakao wilayani hapo Desemba 18, 2023 katika ziara ya kikazi Wilayani Kylea yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mfumo wa
Stakabadhi za Ghala katika zao la Kakao.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Stakabadhi za Ghala Ndg.Asangye Bangua amewataka wakulima kuhakikisha wanapeleka kakao kwenye maghala lakini pia kuhakikisha tunapeleka kakao yenye ubora kwenye ghala na kwa kufanya hivyo kutaongeza kujihakikishia soko la uhakika la kakao.

Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara(Mb) Mhe. Exaud Kigahe akizungumza na Wafanyabiashara walioshiriki kutuma maombi ya kununua zao la Kakao katika mnada wa kakao namba 25 Wilayani Kyela Desemba 18, 2023.

Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.Josephine Manase akizungumza na Wakulima pamoja na wafanyabiashara walioshiriki katika mnada wa kakao namba 25 Wilaya ya Kyela.

MWISHO .