Site icon A24TV News

NAIBU WAZIRI WA KILIMO SILINDE CHUO CHA UHASIBU KULETA MABADILIKO MAKUBWA KATIKA MITAALA YA KIDIGITAL CHUO KINA MAONO MAKUBWA

Serikali imekipongeza chuo cha Uhasibu Arusha kwa kuja na mabadiliko ya mitaala ya elimu katika upande wa kilimo, Biashara ,ufundi,utalii ambayo kwa kiasi kikubwa inayoakisi  mazingira halisi ya  kuisaidia Tanzania katika ukukuzaji wa uchumi.
Akiobgea katika mahafali hayo Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde ameyasema hayo kwa niaba ya Waziri wa fedha  wakati akizungumza katika  mahafali ya 25 ya  Chuo  cha Uhasibu Arusha yenye wahitimu 5387 yaliyofanyika Katika hoteli ya Ngurdoto wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Amesema serikali imewekeza fedha nyingi katika vyuo vya elimu ya kati na vyuo vikuu, kutokana na jitihada kubwa  zinazofanywa na  Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha watanzania wanapata elimu bora na yenye usawa.
“Nafahamu kila mmoja amefanya tafiti kama takwa la chuo kabla ya kuhitimu, ni imani yangu kila mhitimu aishirikishe jamii yake ,na kutokufungia matokeo hayo kabatini, tumieni  utafiti mlioufanya ili  kuongeza tija katika mabadiliko yakiuchumi.”amesema .
Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha (IAA)  Profesa Eliamani Sedoyeka amesema  chuo icho kwa sasa kina jumla ya kozi 71 ambapo 16 stashahada, 17 stashahada, uzamili 14,shahada 24 .
Ameeleza chuo kimeanzisha shahada mpya ya medua bainowai na mawasiliano ya umma, kutokana na mazingira ya Sasa kupitia  msisisitizo wa serikali  katika sekta ya  elimu  yakutengeneza kada ya viongozi katika eneo hilo katika usimamizi wa shule na maafisa elimu ngazi ya wilaya .
“Serikali iliwapatia chuo hiki shilingi   48 bilioni  na mipango ni kukakikisha chuo kinatoa  misingi ya weledi na umahiri  na kuwa kinara  katika maeneo yote , huku mipango mikakati ya miaka 5 ni  kuongeza wigo wa kujenga miundombinu ya kufundishia,kituo cha tehama, kumbi pacha  za kufundishia katika kampasi 4 ya  Arusha,Babati, Dar es salaam, Dodoma na tuna mpango wa kuanzisha kampasi nyingine mpya ya  Songea ambapo  tayari tumepatiwa shilingi  22 bilioni na serikali kwa ajili ya kujengwa kampasi hiyo ili kutengeneza soko lenye uhakika.”amesema.
Hata hivyo ili kuhakikisha usalama wa Raia na mali zao zinalindwa  wameimarisha mahusiano  na chuo cha polisi Moshi kwa kuja na kozi  mbalimbali kwa lengo la kuvifikia vyombo vya ulinzi na usalama.