Site icon A24TV News

BARA BARA SIMANJIRO KITETO AIPITIKI WANANCHI WALIA NA VIONGOZI

Na Mwandishi wetu kiteto

Wanamchi wa Eneo la Nderekeshi wilayani simanjiro  mkoani Manyara wamelalamikia Barabara ya Kiteto Simanjiro kutopitika kwenda mkoani Arusha hali ya barabara eneo ni mbaya wananchi hao ambao asilimia kubwa ni wakulima na wafugaji wameomba viongozi wa mkoa  Manyara Mbunge pamoja na Meneja wa Tan Roads kusikia kilio chao .

Wananchi hao wamesema kwamba  hakutakuwepo na usafiri wilaya hizi mbili Nairero kuna mahali kilimani inataka kukatika jambo litakalo sababisha watu kupoteza maisha .

Kwa sasa mabus yanatokea kiteto yanaingia Arusha usiku saa moja au saa kumi na mbili kuanzia walipo anza safari muda wa saa 12.00 alfajiri.

Bara bara hizo zimesababisha kukosekana kwa mawasiliano ya barabara katika ya kiteto na Handeni eneo la Pori namba moja kiteto barabara ilisombwa na maji  na mpaka sasa hakuna eneo la kupita magari ya Tanga yanaishia pori kwa pori.

Mwisho