Site icon A24TV News

MATAPELI SUGU WA FEDHA ZA MZEE MAEDA WATIWA HATIANI WAFUNGWA KIFUNGO CHA MIAKA 20 JELA TAKUKURU YATOA ONYO KALI,

Na Geofrey Stephen .

Leo tarehe 05,Januari, 2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Shauri la Uhujumu Uchumi ECC. 16/2023 limetolewa maamuzi ambapo Washtakiwa watatu kati ya nane ambao ni A/Isnp.Hillary Ferdinand Komba,PC – Bartholomew Augustine Maya na PC Apornary Proches Burretta wametiwa hatiani na wote kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 kwa kosa la Matumizi Mabaya ya Madaraka k/f Cha 31 Cha Sheria ya PCCA Cap 329 RE 2019 kwa kitendo Cha kufika nyumbani kwa Pro. Maeda na kufanya upekuzi pasipo kufuata utaratibu.

Aidha, washtakiwa watano wameachiwa huru kwa kuwa ushahidi haukuweza kuthibitisha makosa dhidi yao.

Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 19.03.2021 watuhumiwa walikwenda nyumbani kwa Mzee Maeda na kufanya upekuzi kinyume na utaratibu kisha kutumia nguvu kupokea kiasi cha Tshs 73,000,000 kutoka kwa Prof Maeda ili wasimchukulie hatua za kisheria dhidi yake kwa tuhuma ya uongo kuwa alikuwa akimiliki pembe za ndovu. Kitu ambacho hakikuwa cha kweli.

 

Mwisho .