Site icon A24TV News

UMEME SASA WAANZA KUPATIKANA BILA MGAO HALI YAIMARIKA NCHINI

Na Mwandishi wa A24Tv Arusha

kamishna wa umeme na nishati jadidifu,wizara ya nishati anayesimamia sekta ya umeme nchini,mhandisi Innocent Luoga akiongea na waandishi wa habari katika mkutano wa kimataifa wa ushirikiano wa maendeleo ya nishati Afrika unaofanyika jijini Arusha.picha na Anthony Masai.

“yalikuwa ni maelekezo ya mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kuhakikisha umeme unaimarika katika kipindi cha miezi sita”

Serikali imesema hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme nchini inaendelea kuimarika licha ya kuwepo kwa upungufu wa nishati hiyo kwa baadhi ya maeneo ;na kwamba agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa TANESCO kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana ifikapo mwezi Machi 2024,litatekelezeka.

Kamishna wa umeme na nishati jadidifu wa Wizara ya Nishati anayesimamia Umeme nchini ,Mhandisi Innocent Luoga,amesema hayo katika mkutano wa kimataifa wa maendeleo ya nishati uliowakutanisha wadau wa sekta hiyo kutoka nchini mbalimbali Afrika unaoendelea jijini Arusha.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Mhandisi Gisima Nyamhanga,amewataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu wakati masuala ya nishati ya umeme yakiendelea kushughulikiwa.

Mkutano huu unatajwa kwenda kutatua changamoto za nishati ya umeme Afrika kwa kejenga ushirikiano katika maeneo ya uzalishaji na usambazaji.