Site icon A24TV News

ASAKWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MKE WAKE USIKU WA MANANE LOLIONDO.

Na Mwandishi wa A24tv.

kijana mmoja anayejulikana kwa jina la Larinyoni Saitoti Parmeres (28) mkazi wa kijiji cha Lopuluni kitongoji cha Lopoluni A tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro anatuhumiwa kumuua mke wake Nang’ubukule Ikayo Mbalala (20) kwa kumpiga na rungu na kumkata na kitu chenye ncha kali maeneo mbalimbali ya mwili wake kisha kutokomea kusikojulikana.

Akizungumza na maafisa wa shirika la Mimutie linalopambana na kupinga ukatili wa wanawake wilayani Ngorongoro wapofika eneo la tukio mwenyekiti wa kijiji cha Lopoluni Bwn Daniel Kurutut amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jumatano ya Februari 14 2024 ambapo mtuhumiwa baada ya kutenda ukatili huo alitoroka na wao kwa kushirikiana na jeshi la polisi watahakikisha anapatikana na kufikikishwa kwenye vyombo vya dola.

Mashuhuda aliyegundua ukatili huo baada ya kufika nyumbani kwa marehemu akizungumza katika mahojiano na maafisa wa shirika hilo la Mimutie bwn Tomboy Ole Sayori amesema majira ya saa 12 asubuhi mtuhumiwa baada ya kutekeleza unyama huo alichukua hatua ya kumpeleka mtoto wake wa kike mwenyewe mri wa miaka (2) waliyekuwa wakiishi nae kwa mama mzazi wa mtuhumiwa.

Amesema baada ya kumfikisha mtoto huyo alimuacha njee huku yeye akitokomea kusikojulikana ndipo mama wa mzazi wa mtuhumiwa alipogundua uenda kuna tukio limetendaka lisilo la kawaida baada ya kumuona mjukuu wake akiwa ametapakaa damu katika nguo alizokuwa amezivaa

Bwn Tomboy ameendelea kwa kusema kuwa baada ya mama wa mtuhumiwa kuona hivyo ndipo alimpoenda kumuita yeye na kumueleza, huku akichukua hatua ya kwenda kwa marehemu na alipofika na kuingia ndani aligundua marehemu ameuwawa kikatili na mume wake akiwa na majeraha ya kupigwa na rungu (maarufu namba tisa kwa umasaini) maeneo ya kichwani pamoja na kuwa na majeraha ya kukatwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya mbalimbali ya mwili wake.

Kwa upande wake Bwn Isaya Seki mkazi wa kijiji icho akizungumzia tukio hilo amesema mtuhumiwa amekuwa akitishia familia yake kutaka kuua kwani mke mkubwa aliondoka kutokana na kuofia kuuawa na hata alikuwa akimtishia mama yake mzazi kutaka kumuawa.

Alipotafutwa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo kuzungumzia tukio hilo simu yake iliita bila mafanikio huku mtuhumiwa akiwa bado ajapatikana.

Hili ni tukio la pili kutokea wilayani Ngorongoro ndani ya wiki moja kwani shirika la Mimutie liliripoti tukio lingine la kikatili katika kijiji cha Malambo mnamo tarehe 06/02/2024 mwanaume mmoja kwa jina la Lanyori Mathayo (25) alimuua mke wake kwa kipigo baada ya kugoma kuishi nae.

Mwisho.