Site icon A24TV News

MADEREVA WA TANZANIA BARA NA VISIWANI WAPIGWA MSASA KUTUMIA TEKNOLOJIA MPYA,NA JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA CHUO CHA UFUNDI ATC

Na Geofrey Stephen , Arusha .

JESHI la polisi kikosi cha usalama barabarani kwa kushirikiana na Chuo cha ufundi Arusha (ATC) wametoa mafunzo maalumu kwa wakuu wa usalama barabarani na wakaguzi wa magari na watahini wa madereva kutoka mikoa yote Tanzania na Zanzibar kuhusu matumizi ya teknolojia katika usimamizi wa sheria za usalama barabarani.

Akizungumza mkoani Arusha katika mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yanaendelea mkoani hapa,Mkuu wa chuo cha ufundi Arusha ,Prof .Musa Chacha amesema kuwa lengo la mafunzo hayo kwa jeshi la polisi ni kuongeza ujuzi katika ukaguzi wa magari ili watanzania wanaposafiri waweze kuwa salama.

Prof .Chacha amesema kuwa kupitia mafunzo hayo wakuu hayo kwa pamoja wataweza kuwa na uwezo mkubwa wa kutumia teknolojia za kisasa katika kutekeleza majukumu yao.

“Tuna vyombo vya kisasa vya kufundishia udereva katika chuo chetu ambavyo vinasaidia kuwaandaa madereva kuwa watu wazuri ambao wanaweza kufuata sheria za usalama barabarani “amesema Prof Chacha.

Kwa upande wake Naibu Kamishna wa polisi ,ambaye pia ni Kamanda wa usalama barabarani, Ramadhani Ng’anzi amesema kuwa wameweza kupatiwa mafunzo hayo kwa muda wa siku mbili ambapo wamepata uelewa mkubwa sana katika maswala mbalimbali ambayo yatawasaidia kuongeza weledi zaidi kazini.

Ng’anzi amesema kuwa,chuo cha uhasibu Arusha kimepiga hatua kubwa sana katika ufundishaji wa kisasa ambapo wamejipanga kuja na maarifa mapya ya kubuni teknolojia ya magari.

“Kupitia mafunzo haya askari wetu watakuwa na maarifa mengi zaidi na uelewa wa hali ya juu katika kukagua magari kwani katika kutekeleza majukumu hayo ni lazima tuwe na uelewa mkubwa “amesema Ng’anzi.

Naye Mkurugenzi udhibiti usafiri wa barabara, Johansen Kahatano amesema kuwa chuo hiki kimejipanga vizuri katika eneo la kutoa mafunzo hususani kwenye maswala ya usalama barabarani kwani hilo ni eneo sahihi hasa katika eneo la kukagua magari ,hivyo kupitia mafunzo hayo weledi utaongezeka kwa kiwango kikubwa sana.

Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo ambaye ni Mrakibu mwandamizi wa polisi Deus Sokoni amesema kuwa ,washiriki hao wamepata mafunzo kuhusu matumizi ya malipo ya tozo mbalimbali za serikali kwa njia ya kieletroniki (GePG ),pamoja na mfumo wa kisasa wa usajili wa shule za udereva Tanzania.

Aidha amesema kuwa, wameweza kujifunza kuhusu ukusanyaji wa taarifa za ajali za barabarani kwa njia ya kieletroniki, pamoja na ukaguzi wa vyombo vya moto kwa kutumia vifaa vya kisasa.

Aidha watoa mada katika mafunzo hayo ni kutoka Taasisi ya teknolojia ya mitambo Tanzania (IHET),wataalamu wa ICT kutoka Hazina,na wataalamu wa ICT kutoka makao makuu ya jeshi la polisi

Mwisho