Na Richard Mrusha Katavi
Imeelezwa kuwa Hifadhi zilizopo kusini mwa Tanzania zinavivutio vingi lakini hazina umaarufu kama zingine
Afisa Uhifadhi daraja la pili Beatrice Msuya
Amesema hifadhi ya Taifa Katavi pamoja na kutokusikika masikioni mwa wengi imesheeni vivutioa lukuki .
Hayo ameyasema Februari 28,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliotembelea hifadhi hiyo
Amesema vivutio hivyo kuwa ni makundi makubwa ya Simba, Tambo, Nyati, na wanyama wengine, mbali na wanyama hao kuna ziwa zuri na la kipekee ambalo limesheheni viboko Mamba na samaki aina ya Kambare, kamongo.
” hifadhi yetu inasifa ya kuwa na viboko wengi kuliko hifadhi zingine hapa nchini, kwa wingi huo inaiweka kuwa hifadhi namba moja kwa viboko wengi.”
Amesema Msuya kupitia ziwa hilo kuna utalii wa uvuvi wa samaki (spot fishing)
Ambao unakuwa ni sehemu ya kuwachangamsha watalii wanaotembelea hifadhi hiyo na wamekua wakifanya hivyo kwa kushindana kupata samaki mwenye uzito mkubwa kuzidi wengine
Ameongeza kuwa utalii huo wa uvuvi umekuwa chachu kwa hifadhi hiyo ambapo samaki waliovuliwa na kupimwa kisha uachiliwa na kurudi ziwani.
Amesema shughuli za uhifadhi ndani ya hifadhi hiyo zinahusisha kutambua mila na tamaduni za eneo hilo la katavi.
Pia amewaamasisha watanzania kujenga utamaduni wa kutalii haswa kwenye hifadhi ya Taifa Katavi kwasababu ina upekee wa aina yake.
Mwisho.