Site icon A24TV News

PROFESA SEDOYEKA, AMLILIA LOWASA TUTAMKUMBUKA MCHANGO WAKE SHULE ZA KATA,

Na Geofrey Stephen ARUSHA

Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha (IAA)Prof.Eliamani Sedoyeka amemweleza Hayati Edward Ngoyai Lowassa kama kiongozi shupavu aliyeasisi na kusimamia shule za sekondari za kata hapa nchini.

Alisema mchango wa Lowassa katika sekta ya elimu ulipelekea ongezeko la shule hizo hapa nchini aliamini elimu ndio kila kitu kwa maendeleo ya taifa lolote duniani huku kipaumbele chake ni elimu, elimu, elimu.

“Kabla ya kujenga shule za kata hapa nchini kulikuwa na shule elfu moja tu,baada ya kujenga tulifanikiwa kupata shule 3500 hadi 4000,kwa nchi nzima, ukichanganya na shule za binafsi unapata shule 5000″alisema Sedoyeka

Aliongeza kuwa sasa hivi tunawasomi wengi waliopitia shule za kata na wanafanya vizuri,yote hayo ni juhudi za Lowassa

“Shule za kata zimeacha kielelezo kikubwa sana hapa nchini ,mwanzo watu walizifanyia kebehi ila kwa sasa zinafanya vizuri sana, kati ya shule hiyo ni pamoja na shule ya sekondari ya Kisimiri iliyopo wilaya ya Arumeru, ambayo inachuana vibaya sana ”

Alisema Lowassa ataenziwa milele na milele kwa makubwa aliyoyafanya katika taifa hili na atakumbukwa kwa kuwanhakuwa kiongozi anayeyumba ama kuyumbishwa.

………..Ends…..