Site icon A24TV News

RAIS DK. MWINYI ASHIRIKI KHITMA YA MZEE YUSSUF MASAUNI

Na Mwandishi wa A24tv.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki Dua ya khitma ya kumuombea Marehemu Mzee Masauni Yussuf Masauni, Baba Mzazi wa Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe.Hamad Yussuf Masauni ambae amefariki tarehe: 23 Februari 2024 na kuzikwa makaburi ya Mwanakwerekwe tarehe: 24 Februari 2024.

Dua hiyo imefanyika Msikiti wa Fatma Kilimani, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 25 Februari 2024.

Mwisho .