Site icon A24TV News

Serikali yaombwa kutoa elimu juu ya matatizo ya Afya ya akili kwa jamii.

Na mwandi wa A24tv Hai

Siha,Serikali imeshauri kutoa elimu ya matatizo ya Afya ya akili ili jamii iweze kufahamu matatizo wanayopitia yanausiana na Afya ya akili au mambo mengine ili waweze kusaidika

Haya yamejiri wakati wa mafunzo ya siku moja kuhusu matatizo ya Afya ya akili kuwajengea uwezo Jeshi la Polisi Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro ambayo yameandaliwa na Uchumi Bank iliyopo Wilayani humo.

Edward Mwendamseke ambaye ni mwanasaikolojia mtaalamu wa matatizo hayo ,Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyofanyika kituoni hapo amesema elimu itasaidia jamii kufahamu dalili matatizi ya Afya ya akili

“Ni kweli kwa hali iliyopo kwa sasa ni muhimu jamii yetu ijengewe uwezo wakufahamu matatizo ya Afya ya akili wakishafahamu watakuwa na maamuzi sahihi ya kupambana “amesema Mwendamseke

Mwendamseke amesema baadhi ya watu waliopata elimu hiyo wamekuwa wakigundua kuwa baadhi ya changamoto kwenye jamii wanazopitia zinausiano wa moja kwa moja ya Afya ya akili

Kwa hiyo wito wangu viongozi wa Serikali ,Dini, Familia,Shule za msingi na Sekondari kuna haja jamii kupata elimu ya Afya ya akili ili tuweze kujua matatizo tunayoyapitia yanausiana na Afya ya akili au mambo mengine yanayoweza kusaidika.

 

Daniel Nyolobi,Polisi Kata ya Kirua,amesema Jeshi la Polisi linashughulika zaidi na jamii na ishu za kihalifu na ishu za kialifu chanzo ni matatizo ya liyopo kwenye jamii na moja katika matatizo hayo yaliyopo ni pamoja yanayosababishwa na ishu ya Afya ya akili

Kwa hiyo wametuletea wataalamu wa Afya ya akili waweze kufundisha Askari kwa kuwa wanakutana na watu wengi ,elimu hii au maarifa hayayakatumika pia kusaidia jamii kutatua changamoto mbali mbali zinazoweza kusababisha jinai

Jamii inakabiliwa na mambo mengi na wengine kusababisha kujidhuru,sasa ilikuondoka na hali hiyo,Bank ya hiyo imesaidia kuleta wataalamu naamini elimu hiyo sasa ambao Askari kata 17 wamepata itasambaa na itapunguza ama itazuia hali ya uhalifu kuengelea kuwepo kwenye jamii yetu

Meneja wa Bank hiyo Mpoki Mwanjara amesema lengo la mafunzo haya Ni kuponya jamii ambayo itakuwa na maamuzi sahihi ya kuchukua ,
Tanzanian yetu na Wilaya yetu inabaki salama na kupata maendeleo kwa sababu maendeleao ni jambo la akili

 

Mkuu wa jeshi la Polisi Wilayani humo Zakia Shuma,amesema wamepata elimu na wataipeka kwa jamii kupitia polisi kata ,kwani jamii inamatatizo madogo madogo ,labda aneshindwa kuimudu familia mwingine aneshindwa kujiamini kwenye maisha

Amesema kwa siku tatu wamepata vifo vitatu kwa siku Kama nne hivi kwa watu kunywa sumu ni jambo la hatari kwa hiyo hii elimu inatujenga sisi jeshi la Polisi na pia tunakwenda kuitoa kwa jamii

Mwisho