Site icon A24TV News

SMZ KUPUNGUZA GHARAMA ZA VYAKULA

Na Mwandishi wa A24Tv .

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itapunguza gharama za vyakula nchini.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya sala ya Ijumaa Msikiti wa Mubarak Bububu Kihinani, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 23 Februari 2024

Rais Dk.Mwinyi amesema atatoa taarifa muda mfupi ujao katika kukabiliana na hali ya upandaji wa gharama za vyakula ili kuwapunguzia mzigo wananchi.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amewahimiza waumini kutenda mema kwa kudumisha amani na kuwasaidia makundi ya wasiojiweza katika kuelekea kipindi cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Mwisho .