Site icon A24TV News

Tani 18.6 za mahindi zatolewa kwa waliokumbwa na mvua za mawe Hai

Na Mwandishi wa A24tv.

Serikali wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro imetoa zaidi ya tani 18.6 za mahindi ya chakula kwa waathirika wa mvua ya mawe ya barafu iliyombatana na upepo mkali katika baadhi ya kata za Wilaya hiyo na kuathiri zaidi ya ekari 20 za migomba ya ndizi, mahindi, parachichi pamoja na nyumba zaidi ya 15.

Hai.Serikali wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro imetoa zaidi ya tani 18.6 za mahindi ya chakula kwa waathirika wa mvua ya mawe ya barafu iliyombatana na upepo mkali katika baadhi ya kata za Wilaya hiyo na kuathiri zaidi ya ekari 20 za migomba ya ndizi, mahindi, parachichi pamoja na nyumba zaidi ya 15.

Mjumbe kutoka Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Akizungumza Gaspar Ijiko kwenye kikao cha kawaida Baraza la madiwani halmshauri ya Hai mkoani hapa

Mvua hizo ambazo ziliambatana na upepo mkali zilianza kunyesha Januari 19, mwaka huu kuanzia saa tisa mchana ambapo ilidumu kwa zaidi ya saa moja na kuleta taharuki kubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo baada ya upepo kuangusha miti mikubwa, kahawa, migomba na mahindi yaliyokuwemo mashambani ambapo majani ya migomba na mahindi yalichanwa chanwa na mvua hiyo ya mawe.

Hata hivyo kata zilizoathirika zaidi na mvua hizo ni kata za Machame Mashariki, Kaskazini na kata ya Masama Rundugai ambapo wananchi wa maeneo hayo waliathirika zaidi na mvua hizo

Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Amiri Mkalipa Akizungumza kwenye Baraza la kawaida la madiwani halmshauri hiyo

Akizungumza, Kaimu Mkurungenzi wa halmashauri hiyo, Rajabu Yateri amesema baada ya kutokea maafa hayo serikali ilifanya tathmini ambapo kwa sasa wameanza kutoa msaada wa vyakula kwa waathirika hao.

“Tunaishukuru Serikali kwa kutupatia tani 18.6 za mahindi ya chakula kwa waathirika wa mvua zilizotokea hivi karibuni, utaratibu wa ugawaji wa mahindi haya utatolewa kwa wananchi,”amesema Rajabu

Amesema kata za Machame Mashariki, Kaskazini na Masama Rundugai ambazo ndizo zilizoathiriwa na mvua hizo ndizo zitakazopatiwa msaada wa chakula hicho.

Naye, Diwani wa viti maalumu, Hausem Nkya ameishukuru serikali kwa kutoa msaada huo na kusema jamii nyingi zilikuwa zina hali mbaya baada ya mazao yao kuharibiwa na mvua hizo

“Tunaishukuru serikali kwa kutupatia msaada huu mkubwa, imetupa matumaini makubwa sana, maana wananchi wetu walikuwa hawana chochote baada ya mazao yao kuharibiwa na mvua za mawe,”

Pamoja na shukrani hizo pia ametoa ombi kwa serikali kuangalia namna ya kuwasaidia wala ambao nyumba zao ziliharibiwa na mvua hizo na kuwaacha bila makazi.

 

Mwisho.