Site icon A24TV News

Wanawake burunge WMA wasaidiwa

Mwandishi wetu.babati

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo amewahamasisha Viongozi wa vikundi 10 vilivyomo katika eneo la jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapiri ya Burunge kuhifadhi kumbukumbu zao za fedha Kwa usahihi ili kuepusha migogoro itakayosababisha vikundi hivyo kuvunjika.

Ameyasema hayo Leo February 7 wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu Kwa Viongozi wa vikundi hivyo, iliyoandaliwa na Taasisi ya Chemchem Association inayofanya shughuli za uhifadhi katika Jumuiya ya Hifadhi Burunge iliyopo mkoani Manyara.

amesema kuwa baadhi ya mambo yanayosababisha vikundi kuvunjika ni pamoja na kuto kutunza kumbukumbu Kwa usahihi na kutumia fedha za kikundi bila utaratibu
amewataka Viongozi hao kuto kuhifadhi fedha majumbani na badala yake kufungua akauti ya kikundi bank kulingana na sera ya fedha ya jamii ya Mwaka 2019 inayota kila kikundi kuwa na akaunti ya benki.

“Serikali inathamini sana vikundi vya kuweka akiba na kukopa kwani vikundi vinachochea maendeleo ya jamii hivyo Viongozi wa vikundi mnapaswa kuwa waaminifu Kwa pesa za kikundi ili kujenga Imani Kwa wanakikundi.” alisema Mkurugenzi huyo.

Awali akimakaribisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Babati, Meneja Mkuu wa Chemchem Association Clever Zullu amesema kuwa wanajivunia sana kuwezesha vikundi hivyo kukopesheka na furaha Yao ni kuona matunda ya uhifadhi unaoongozwa na wananchi wenyewe yanakuwa na manufaa makubwa.

Amevitaja vikundi 10 vinavyosimamiwa na Chemchem Association kuwa ni Upendo -B, Marewa, Kigogoni, Datoga, Wacheda,Keja, Esinyati, Mdorii, Upendo -A na Mang’oo ambapo Viongozi wa vikundi hivyo watapatiwa mafunzo ya siku tatu ili kuendana na Sera ya Community Microfinance ya 2019 ambavyo vitasajiliwa na kutambuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Babati.

Mkurugenzi wa Chemchem Association Bi Fabian Bausch amesema kuwa Umoja na mshikamano kati ya vikundi vya kuweka na kukopa vimewezesha kuwakwamua kiuchumi wakazi wa vijiji kumi vinavyozunguka Jumuiya ya Hifadhi Burunge.

Amesema wakati wanaanzisha vikundi hivi mwaka 2017 Kwa kila Kijiji jamii haikuwa na uelewa mkubwa juu ya kuwa na vikundi vya kuweka na kukopa lakini Kwa Sasa Dunia nzima inafahamu shughuli za uhifadhi zinazofanywa Juhibu na kuwavutia wageni wengi wanaokuja kutali na kuongeza fedha nyingi za kigeni.

kupitia fedha hizo Chemchem Association inatejesha Kwa jamii Kwa kusaidia KATIKA sekta za elimu, Afya na mazingira

mwisho