Site icon A24TV News

BAKWATA Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro waomba Serikali kuzipa uwezo Hospitali za Wilaya na mkoa

Na Mwandishi wa A24Tv .

BAKWATA Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro waomba Serikali kuzipa uwezo Hospitali za Wilaya na mkoaBaraza kuu la WaislamuTanzania (BAKWATA), Wilayani siha mkoani Kilimanjaro,limeitaka Serikali kuweka mkakati thabiti ya kuzipa uwezo Hospitali za ndani ikiwamo za Wilaya na mkoa ili kupunguza gharama kwa Wananchi kwende kufuata matibabu sehemu nyingine ikiwamo nje ya Nchi.

Kauli hiyo imesemwa na Ramadhani Mollel katibu wa Baraza hilo wakati Viongozi wa BAKWATA Wilaya pamoja na waumini walipotembelea nyumbani Sheikh wa mkoa huo Shaabani Mlewa Mara baada ya kurejea Nchi kutokea India alilokuwa kwa matibabu ya macho

Akizungumza nyumbani kwe Sheikh Bomang’ombe Wilayani Hai mkoani hapa Mara baada ya kumjulia hali,amesema kuna haja kuzijengea uwezo Hospitali za Wilaya na mkoa ili kupunguza gharama za watu kufuata huduma za matiba maeneo ya mbali ikiwa nje ya Nchi.

 

“Ni kweli gharama za matibabu ni kubwa hasa kwa magonjwa kama ya moyo na sukari na prsha ,ushauri wangu Serikali iboreshe Hospitali za Wilaya na mkoa ili kupunguza changamoto hizo kwa Wananchi”amesema Mollel

Amesema baadhi Wananchi wamekuwa wakitaabika kwa gharama kubwa wakihangaika kutafuta michango ya kupata fedha kwenda kuwakomboa ndugu zao baada ya kushindwa kulipa fedha kwa baadhi ya Hospital baada ya matibu ,lakini kama Serikali itazijengea uwezo Hospitali hizo wananvhi wata epukana na kadhia hiyo

Aidha amewashukuru wadau mbali mbali na wale wote waliofanikisha matibabu ya Sheik akiwa Nchin India akiwamo Rais Samia Suluhuu Hassani na mbunge wa Rombo, nakuomba waendelee na moyo huo wakisaidia

“Ni kweli kuwashukuru wale waliomsaidia Sheikh kupata matibabu na kurejea Nchini ni jambo muhimu sana kwani hakuna la kuwapa zaidi ya shukran “amesema Mollel

Kwa upande wake Sheikh Mlewa , amesema kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kukaa Nchini India takiribani miezi 5 kwa matibabu ya macho gharama ni kubwa ,na kuwashukuru wale wote walimuwezesha kupata matibabu hayo

“Ni kweli nachukua frusa hii kushuka Rais Samia Suluhuu Hassani,namshuru zaidi,Mufti wa Tanzaniania Abubakar Zuber,Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda na wele wote walioshiriki kunisaidia Mwenyezi Mungu atawalipa “amesema Mlewa

Aidha Ally Muhamedi Immamu wa Msikiti wa SanyaJuu Wilaya humo,amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la maradhi yasiyoambukiza kwa maana ya kisukari ,Presha ,Moyo na figo yamekuwa ni magonjwa hatari na gharama ya matibabu ni kubwa

Hivyo kuwashauri Waislamu na Wananchi kwa ujumla kuzingatia kufuata utaratibu wa wataalamu wa Afya kuhusu ulaji wa vyakula vinavyofaa,hata Dini ya kiislamu inazungumzia swala la kula kwa kufuata utaratibu ili kulinda afya , hivyo kuomba utaratibu kuzingatiwa

Mwishoni